TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Al Hilal mjini Khartoum nchini Sudan.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Mghana Augustine Okrah dakika ya 19, Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 26 na Mzambia Clatous Chama mawili, moja kwa penalti dakika ya 42 na lingine dakika ya 55, wakati ya Kotoko yamefungwa na Steven Mukwala dakika ya tisa na Stephen Amankona dakika ya 79 kwa penalti.
Simba itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na wenyeji, Al Hila kabla ya kurejea nyumbani kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya AS Arta Solar ya Djibouti Septemba 3.