Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia, Dar es Salaam
Licha ya jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kuhakikisha waliokidhi vigezo wanapata namba za Nida/ au vitambulisho kwa haraka lakini kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watu kujisajili zaidi ya mara moja na wengine kutoa taarifa zisizo sahihi hali inayopelekea kuleta usumbufu wakati wa uhakiki .
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam January 10 ,2025 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchi Daniel Sillo mara baada ya Ziara yake ya kikazi ya kutembelea kituo cha kuchakata taarifa Makao Makuu ya Mamlaka Vitambulisho vya Taifa NIDA ambapo amewasihi wananchi kuwa wale wote wanaohitaji Vitambulisho wapeleke taarifa sahihi zinazowahisu ili kupunguza changamoto ya kuchukua muda mrefu wa kuhakiki taarifa zao na wapate Vitambulisho kwa haraka.
” Niseme kuwa Utakuta mtu mmoja anajisajili zaidi ya mara moja Leo jina hili kesho jina lingine mtambue kuwa Vitambulisho vya Taifa ni usalama wa Utaifa ni lazima kabla ya kutoa kitambulisho zoezi muhimu la uhakiki wa taarifa lifanyike na kwa kutumia muda mrefu kidogo hivyo ni Jambo la muhimu wale wote wanaohitaji Vitambulisho wapeleke taarifa sahihi zinazowahisu ili kurahisisha uhakiki wa kutumia muda mfupi na kitambulisho kitoke kwa wakati” amesema Naibu Waziri Sillo
Sambamba na hayo ameipongeza NIDA kwa kuchukua hatua kuwaandikia wananchi ujumbe wa simu(SMS) wale wote ambao hawajachukua Vitambulisho na kuwaambia Vitambulisho vya tayari vimeshatoka na wakachukue ofisi gani hivyo amewasihi watu wote ambao hawajapata Vitambulisho waende mahali walipojisajili .
Hata hivyo ameipongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kutoa fedha billion 42.5 kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wote wanapata Vitambulisho vya Taifa pia amewapongeza NIDA wa jitihada zao ambapo kuanzia Mwezi Septemba 2023 uzalishaji mkubwa wa Vitambulisho lifanyike na tayari wameshasambaza Vitambulisho Million 20 kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA James Kaji amesema kumekuwa na changamoto zinazosababishwa na wananchi wenyewe katika upatikanaji wa Vitambulisho hivyo amewaomba wale wanaofikisha miaka 18 kuanzia zoezi la kujisajili mapema wasisubirie mpaka wanapofikia vyuo au wakati wa kuomba ajira hali inayopelekea kuwa na wingi wa watu katika vituo kupata huduma
Pia amewasihi wale ambao wajisajili majina yanayoendana na shule au vyeti vya kuzaliwa kwani kumekuwa na wimbi la watu walioachishwa kutokana naajina feki hivyo ni vyema kuepuka kadhia hivyo mapema.