đź“ŚMatumizi ya wakandarasi wasio na utaalamu (Vishoka)kutandaza nyaya (wiring)pasipo kuwa na utaalaamu wa kufanya hivyo
đź“Ś*Matumizi holela ya vyombo mbalimbambali vinavyohitaji kutumia nishati ya Umeme visivyotengenezwa kwa ubora
đź“ŚMatumizi Mabaya ya Nishati zingine vyatajwa kuongoza kama chanzo cha majanga ya moto nchini
Kamanda wa Jeshi la zima moto na Uokoaji Mkoani Geita, Kamanda Mratibu Hamis Dawa,amesema kuwa majanga mengi ya moto yanayozuka majumbani hayasababishwi na umeme unaotoka TANESCO bali nimatumizi holela ya vyombo vya umeme pamoja Na kutochukua tahadhari ya vifaa bora na Mkandarasi sahihi aliyehakikiwa kwaajili ya kutandaza nyaya katika nyumba zao.
Kamanda Mratibu Hamis Dawa ameyasema hayo Mei 24, 2024 alipotembelea Banda la TANESCO , katika maonesho ya Biashara ,Viwanda na Kilimo yanayoendelea mkoani Geita.
Amesema mara nyingi inapotokea moto majumbani au viwandani cha kwanza wananchi ni kutupa lawama kwa umeme wa TANESCO kama chanzo cha moto huo, kabla ya kusubiri ripoti ya uchunguzi kutoka katika Jeshi hilo.
Aidha amesema kuwa jukumu la TANESCO ni kupeleka Umeme kwa Mteja mpaka kwenye mita lakini suala la Umeme ndani ya nyumba ni suala la Mteja kuhakikisha Nyaya ndani ya nyumba yake zimetandazwa vizuri, na vifaa vyote vilivyotumika vinaubora ikiwemo saketibreka.
Akizungumzia matumizi holela ya vyombo vinavyohitaji nishati ya umeme yanayoweza kupelekea majanga ya moto Kamanda Mratibu Hamis amesema kwamba ni muhimu kwa watumiaji Umeme kuhakikisha wanatumia vifaa vya Umeme vyenye ubora kwa umakini na kuzima kila baada ya kutumia vifaa hivyo
“Kuna vifaa vingine vya Umeme vinaweza kujizima vyenyewe baada ya kutumia Umeme kwa kiwango kinachotakiwa (energy efficiency)na vina uwezo wa kudhibiti Umeme , vifaa hivyo ni kama Ac na Friji, lakin vifaa kama pasi na jiko,unaposahau kuzima baada ya matumizi vinaweza kuwa chanzo cha moto, na utasema tatizo ni Umeme wa TANESCO lakin chanzo ni matumizi holela yasiyozingatia utaratibu sahihi wa kuvitumia” amesema Kamanda Hamis Dawa
Ameongeza kwa kusema kuwa katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia, Jeshi la Zimamato na uokoaji, limeanza kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Nishati safi ya kupikia ikiwa ni Nishati ya Umeme na gesi ili kuepusha majanga ya moto.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Mhandisi Joachim Ruweta, amesema kuwa TANESCO Mkoa wa Geita inashirikiana kwa ukaribu na Jeshi la zima moto na Uokoaji, mkoani humo , kwa kufanya kazi kwa kushirikiana kwani kazi zao zinategemeana.
“ Tunafanya kazi kwa ushirikiano sana na Jeshi la zima moto hapa mkoani Geita, wanapopokea Taarifa ya moto, wanatupigia na sisi ili twende kuzima Umeme, kwasababu kuna kemikali zingine wanazozitumia , haziendani na Umeme, hivyo wao hawawezi kuzima moto bila kutushirikisha” amesema Joachim.
Akihitimisha Joachim ametoa rai kwa wananchi kutumia vifaa vya umeme kwa umakini, na kukagua njia za umeme ndani ya nyumba zao kila baada ya miaka 5, ili kuepuka matatizo mbalimbali ya imeme kama upotevu wa umeme, na majanga ya moto.