Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Dodoma
Katika kukimarisha afya ya akili na mwili kwa wanafunzi shule ya Awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu jijini Dodoma, imeanzisha somo la mchezo wa karate.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Evarist Runiba, amesema hayo jana wakati akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya darasa la saba ya shule hiyo.
Amesema michezo hiyo ni sehemu ya kuwasaidia kuimarisha afya za wanafunzi wao ili kufanya vizuri katika masomo yao na shunguli mbalimbali za kila siku.
“Shule yetu pamoja na kufundisha masomo mengine lakini pia tunafundisha lunga ya kichina na kifaransa lakin pia tunalo darasa la mchezo wa karate ambalo wanafnzi wote wanapata mafunzo wakiwa hapa shule”amesema.
Amesema katika amchezo huo wa karate wanao walimu waliobobea katika mchezo huo hali ambayo itasaidia wanafunzi hao kuwa timamu kimwili na kiakili ili kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.
Mgeni rasmi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, alisema amefurahishwa na vipaji mbalimbali alivyoona kwenye shule hiyo.
Amesema ni vyema shule zingine ziige mfano huo kwa kutenga muda mzuri wa wanafunzi kucheza na kuimba.
Aidha, amesema kuna wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kama vilivyoonekana kwenye mahafali hayo na kwamba kama vipaji hivyo vikiendelezwa wanaweza kupatikana wasanii wakubwa nchini.
“Mnafanya vizuri sana na muendelee hivyo hivyo kwenye michezo na burudani kwasababu hawa wameonyesha vipaji vya aina yake natoa wito kwa shule zingine ziige,” amesema
Aidha, amesema michezo inawafanya wanafunzi wanakuwa na afya njema hali ambayo pia itachangia kufanya vizuri kwenye masomo na mitihani yao pia hivyo walimu wasione kama michezo ni kupoteza muda bila sababu.
“Mbalina masomo ya kawaida wapeni muda wa kucheza kuonyesha vipaji vyao, hawa lazima wapate muda wa kufanya mambo mengine yanayowapa furaha kama michezo,” amesema.
Wanafunzi hao walionyesha umahiri mkubwa kwenye kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali hali ambayo iliwafurahisha wageni na wazazi waliofika kwenye mahafali hayo ambapo wengine walikuwa wakiwatunza.