Na Isri Mohamed
Rapa wa kike kutoka Afrika Kusini, Sho Madjozi ametangaza rasmi kuachana na muziki mara tu baada ya kuachia albamu yake.

Sho Madjozi amethibitisha hilo akiwa kwenye mahojiano na kituo cha SABC News Online, ambapo amesema.

“Ndio naachana na muziki na album yangu inayofuata ndio itakuwa ya mwisho, Nina sababu nyingi za kuacha lakini kubwa zaidi ni kuwa nimeshafikisha ujumbe wa Kila kitu nilichopanga kufikisha kupitia muziki”

“Nimefikisha ujumbe kuhusu Tamaduni, lugha na Masuala ya wanawake, hivyo nadhani nimeshafanya Kila kitu nilicholenga kufanya”

Sho Madjozi amewahi kufanya ngoma kadhaa na wasanii wa Bongo akiwemo Darassa na Marioo.