Kwa kuwagusa wananchi wa maeneo ya vijijini Tanzania, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameonyesha njia na kuongoza kwa vitendo mapambano dhidi ya adui maradhi katika nchi yetu.
Baada ya kufanyika kambi ya huduma za afya kijijini Pohama kwa siku tano ambapo mgeni rasmi Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, na alihudhuriwa pamoja na maelfu ya wananchi kutoka mikoa ya Singida na Manyara.
Pia kwa kushirikisha madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa-Singida, Hospitali ya Rufaa-Mount Meru, Arusha na madaktari na wahudumu wa afya kutoka Wilaya ya Singida na madaktari kutoka USA nchini Marekani waliokuja nchini kupitia Shirika la STEMM.
Katika kambi hiyo zaidi ya wagonjwa 2,020 walitibiwa na kupewa dawa na huduma za kitabibu bure bila malipo yeyote.
Aidha,uongozi wa Mkoa wa Singida, chini ya uongozi shupavu wa Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba pamoja na RMO na DMO-Singida DC, wamefanya kazi na kuwa mfano wa watenda mema katika Taifa letu.
.