Na Lookman Miraji, JamhuriMedia,Dar es Salaam
Michuano ya kimataifa ya mchezo wa kricket katika kampeni ya kufuzu kombe la dunia kwa upande wa mchezo wa kricket yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini kuanzia Septemba 20, mwaka huu.
Mashindano hayo yatafanyika nchini yakijumuisha jumla ya mataifa sita ya Afrika ambayo ni Tanzania, Cameroon, Mali, Lesotho, Malawi pamoja Ghana.
Mashindano hayo yatafanyika ili kupata timu mbili za juu ambazo zitaendelea katika hatua inafuata ambapo zitaungana na timu nyingine mbili kukamilisha idadi ya timu nne ambazo zitachuana katika hatua ya fainali ili kuzipata timu mbili zitakazowakilisha bara la Afrika katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2026.
Mashindano hayo ya kricket yataanza kufanyika nchini kuanzia Septemba 20 mpaka septemba 26 mwaka huu.
Kombe la dunia la mchezo huo litafanyika nchini Sri Lanka pamoja na India kuanzia mwezi Februari mpaka Machi mwaka 2026.