Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dr Seif Shekalage amezitaka asasi za kiraia nchini kuwa waadilifu, wawazi wenye nidhamu ya pesa zinazotolewa na wafadhili kwa ajili ya usimamizi wa miradi, wakifanya shughuli zinayoendana na pesa zinazotolewa ili kuwajengea imani na kupewa miradi mingine kusimamia.

Rai hiyo ameitoa Novemba 8,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi mpango kazi wa Ujanibishaji (Localization) ulioandaliwa na Shirika la Save the Children uliolenga kufanya juhudi za maendeleo kwa kuwafikia moja kwa moja watoto hususani wenye mahitaji kwa kuzijengea uwezo asasi za kiraia nchini Tanzania.

Dr Shekalage amesema kuwa ili kufikia malengo ya miradi inayoanzishwa ni muhimu kuwashirika wananchi na kujua vipaumbele vyao ndani ya jamii inayowazunguka hapo ndipo matokeo mazuri na endelevu ya miradi yatakapopatikana .

” Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan inatambua sana mchango wenu na shughuli mnazozifanya ndiyo maana nawekeza kwa watoto na , imeanzisha idara maalum ya watoto katika usimamizi wa sera na sheria huku akiweka elimu bure ,imeboresha sekta ya Afya, matibabu bure kwa watoto lengo la kuandaa Taifa la kesho” amesema Dr Seif

Sambamba na hayo amewataka watoto kuzingatia maadili mwema wanayofundishwa na wazazi wao, pamoja na kuzingatia masomo yao na kujiepusha vitendo visivyofaa yanayoweza kubadilisha ndoto zao.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania amesema kuwa safari yao imenza miaka kadhaa na wamefanya kazi kwa kutambua kuwa matatizo au changamoto zinazohusu watoto Tanzania ni nyingi na hawawezia kufika na kuzipatia ufumbuzi wenyewe hivyo ni budi washirikiane na wadau mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia na tasisi za kiserikali.

Naye Mkurugenzo wa Usimamizi miradi Save the children Tanzania Anator Rugeikamu amesema Mpango huo mkakati waliouzindua watahakikisha wanafanya kazi ya kuwajengea uwezo wadau wao ikiwemo Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ili lengo lao la kuhakikisha kila mtoto anajengewa mazingira salama ya kiafaya, kielimu, kiulinzi na kupata haki zake za msingi.

“Licha ya Shughuli zinazofanyika lakini mara nyingi mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na changamoto ya kupata raslimali fedha kimsingi changamoto ya kwanza ni kufikiri kasumba kuwa hawana uwezo mifumo inayoweza kusimamia kwa uthabiti pesa za wafadhili zinazoweza kuwafikia walengwa wanaowahudumia ” amesema Anator

Aidha ili kuweza kutatua suala hilo ni budi kuwajengea uaminifu na uwazi kuhakikisha wanakuwa mifumo na utawala ulio huru ana bodi ambayo ni huru itakayoaminika .