Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Temeke
JUMUIYA ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa, Sheikh Dkt. Alhadi Mussa Salum ameipongeza Taasisi binafsi ya Wanawake Laki Moja kwa kudhamini Tamasha Ligi ya Wanawake yenye kauli mbiu: ‘Cheza kama Mwanamke, Soka ni ajira’ inayofanyika katika uwanja wa Buliyaga Temeke.
Sheikh Dkt. Alhadi Mussa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa ligi hiyo Januari 25, 2025, amesema michezo ni afya na inaleta umoja na inapaswa kuungwa na wadau wote katika kusaidia ajira kwao na kwa Taifa.
“Ninawapongeza Wanawake Laki Moja kupitia kwa Mlezi wake Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Mh. Tano Mwera.
Lakini pia qaandaaji wa michezo hii nimefahamishwa wapo viongozi ambao walikuwa wachezaji wa mpira wa miguu wa wanawake pia. Niwashukuru wanamichezo wote na wana Temeke, nawasapoti na tupo pamoja katika kuungana mkono ilikuwafanya wachezaji wetu hawa wanaendelea mbele zaidi.” amesema.
Aidha, katika tukio hilo mgeni rasmi amekabidhi zawadi maalum pamoja na kukagua timu sambamba na kufungua rasmi michezo hiyo kwa kupiga mkwaju wa penati, aliweza ujaza wavuni mkwaju huo kwa kupoteza golikipa aliyerukia upande wa kulia na mpira kuingia wavuni upande wa kushoto.
Kwa upande wake DC Mstaafu Mhe. Tano Mwera amewashukuru wadau akiwemo Dkt. Alhadi Mussa Salum na JMAT kwa ujumla kwa kuitikio wito wa ugeni rasmi, pia amewashukuru viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa na wadau pamoja na Wananchi.
“Tukio hili la kihistoria kwa soka la Wanawake Tanzania, nimshukuru mgeni rasmi kwa kufika.
“Mimi kama mdhamini wa Wanawake Laki Moja, nilipokea barua kutoka kwa Salum Nonji Makamu Mwenyekiti wa soka Wanawake Temeke, Mwanaidi Kingwndu mchezaji wa zamani wa soka la Wanawake waliniomba kudhamini na kwa umuhimu wake wakalipa jina la Wanawake Laki Moja Cup 2025.
Taasisi yetu ipo nchi nzima Tanzania Bara na Visiwani. Tunaamini kupitia ligi hii itaamsha hali ya kuelimisha jamii kupenda mchezo wa soka kwa Wanwake kama soka ni ajira na sio uhuni.” Amesema DC Mstaafu Tano Mwera.
Kwa upande wake Mratibu wa ligi hiyo, Mwanaharusi Kingwendu golikipa wa zamani wa Simba Queens, Yanga princess na Twiga Stars ya Wanawake, amesema timu Nne za Sayari Queens, Evergreen Queens, Masala Princess na Temeke Sisters wanashiriki kwa mfumo wa mtoano na baada watapata timu zitakazocheza fainali.
Nae Salum Mnonji ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Temeke , amesema mchezo huo wa soka la wanawake umekuwa na msisimko katika Wilaya hiyo hivyo wamewaomba wadau wajitokeze katika ligi hiyo ikiwemo siku ya fainali.