Shambulizi la usiku kucha la Urusi katika eneo la kati mwa Ukraine, Poltava limeharibu miundo mbinu ya nishati na kukata umeme kwenye makazi 20. Haya yamesemwa leo na mamlaka katika eneo hilo.
Shambulizi la usiku kucha la Urusi katika eneo la kati mwa Ukraine, Poltava limeharibu miundo mbinu ya nishati na kukata umeme kwenye makazi 20. Haya yamesemwa leo na mamlaka katika eneo hilo.
Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, gavana wa eneo hilo Filip Pronin, amesema taka kutoka kwa droni zilizoanguka, ziliharibu nyumba kadhaa, lakini hakukuwa na majeruhi.
Katika mji wa kaskazini mashariki wa Zaporizhzhia, shambulizi la jana Jumatatu lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi takriban watu saba. Haya ni kwa mujibu wa gavana wa eneo hilo Ivan Fedorov.
Wakati huo huo, jeshi la anga la Ukraine limesema limedungua droni 66 lakini likapoteza mwelekeo wa droni nyingine 13 kati ya 81 zilizorushwa na Urusi wakati wa shambulizi hilo la usiku kucha ambalo pia lilihusisha kurushwa kwa makombora.