UKRAINE imekuwa ikikabiliana na uvamizi wa Urusi kwa zaidi ya miaka miwili na nusu. Urusi imekuwa ikiyashambulia maeneo ya Ukraine wakati wa usiku kutumia makombora ya masafa marefu.
Mabaki ya droni za Ukraine yaliyokuwa yakianguka yamesababisha moto katika kituo cha viwanda eneo la Kaluga kiasi kilometa 200 kusini magharibi mwa mkuu wa Urusi, Moscow.
Gavana wa eneo hilo Vladislav Shapsha amesema hivi leo kwamba hakuna majeraha yaliyotokea na kwamba droni tatu za Ukraine zimeharibiwa. Hata hivyo hakusema ni kituo kipi kilichokuwa kikichomeka.
Wakati haya yakiarifiwa, meya wa mji wa Kiev Vitali Klitschko amesema mifumo ya ulinzi wa anga ilikuwa ikifanya kazi jana jioni kufuatia shambulizi jipya la droni kutoka kwa Urusi.
Jeshi la Ukraine limesema awali mfumo wa ulinzi wa anga wa mji wa Kiev ulizitungua droni 50 kati ya 73 zailizorushwa na Urusi kuyalenga maeneo mbalimbali usiku kucha kuamkia Jumamosi iliyopita.