Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dodoma
Serikali imekutana na uongozi wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kutokana na malalamiko ya wafanyakazi juu ya nyongeza ya mishahara ya kima cha chini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa kilikuwa kati ya viongozi wa TUCTA na Serikali.
“Napenda kuwajulisha kuwa tumekutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na baada ya mazungumzo ya awali viongozi hao waliomba wapate muda wa kwenda kujadiliana na baadaye watakuja kuzungumza na Srikali.
“Kwa hiyo mazungumzo hayo tayari yameanza na viongozi wa TUCTA watakapokuwa wamekamilisha majadiliano yao watakuja kukutana na Serikali ili tusikilize hoja zao na baada ya hapo tutatoa maelezo ya Serikali.
“Kama mtakumbuka juzi baada ya wafanyakazi kuonesha kwamba hawajaridhika na nyongeza ya mshahara iliyoanza Julai mwaka huu ,Serikali ilitoa ufafanuzi na kuahidi kwamba leo ingekutana na wafanyakazi kwa maana ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi ,” amesema.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamuhokya amesema,wamekutana na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuonyesha namna gani ambavyo hawajaridhika na nyongeza ya mishahara iliyoahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu.
Akizungumzia kuhusua nyongeza ya mshahara wa kima cha juu amesema,wapo waliuopata kuanzia sh.8,000 hadi sh.12,000 jambo ambalo amesema haiwezekani mtu kutumia Taifa kwa miaka mingi halafu aongezewe kiasi hicho cha fedha kwamba ndio nyongeza ya mshahara.
“Tulitetemea nyongeza hiyo ingewagusa wafanyakazi ngazi zote kwa kiwango kama ilivyozoieleka,na kwa asilimia aliyoingeza Rais ni kama sh.70,000 hivi lakini imekuwa tofauti.
“Mei Mosi mwaka jana mkoani Mwanza ,na mwaka huu hapa Dodoma Rais Samia alituambia anatakeleza ahadi hiyo katika bajeti inayoanza Julai Mosi mwaka huu ,na wafanayakzi walisubiri kwa hamu na walikuwa na furaha na bashaha lakini imekua tofauti na matarajio yao.
Amesema,wanaamini Serikali wamelipokea na watalifanyia kazi na kwamba bado wanasubiri majibu ambayo watayarudisha kwa wafanyakazi.