………………………………………………………………………………………

Serikali imeunda kamati yenye wajumbe nane ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando kwa ajili ya kutathimini hali ya vyombo vya habari .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24,2023 na waandishi wa habari,Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa kamati hiyo imepewa muda wa miezi mitatu kukamilisha kazi hiyo.

Amesema kuwa kamati hiyo imepewa majukumu ya kufanya kutathmini pamoja na kupata taarifa ya hali ya vyombo vya habari kiuchumi na kiutendaji,kupata taarifa ya hali ya waandishi wa habari katika vyombo vya habari kwa ujumla.

Vilevile amesema majukumu mengine ya kamati hiyo ni kutathimini juu ya sababu ya changamoto katika vyombo vya habari lakini pia kupendekeza njia bora za kukabiliana na changamoto hizo.

Pia amewataja wajumbe wengine wa kamati hiyo kuwa ni msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ambaye pia ni Katibu wa Kamati hiyo, Bakari Machumu kutoka Mwananchi Communication,Dkt.Rose Reuben Mkurugenzi wa TAMWA na Joyce Mhaville kutoka ITV.

Wengine ni Richard Mwaikenda kutoka Blog ya Taifa ya CCM ,Sebastian Maganga kutoka Clouds Media,Kenneth Simbaya Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC ) na Jacquiline Woiso kutoka Mult choice Tanzania.