Waziri wa Kilimo Hussen Bashe ametoa Trekta tano kwa vijana na wanawake katika Wilaya wa Njombe kwa ajili ya mradi wa Kilimo cha jenga kesho iliyo bora (BBT) ili kurahisha shughuli hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakissa Kasongwa amesema hayo wakati akizungumza na vijana na wanawake ambao wamejiunga na mradi huo katika Halmashauri tatu Halmashauri ya Mji makambako,Halmashauri ya Wilaya ya Njombe vijijini pamoja na Halmashauri ya mji Njombe.

Mkutano huo ulio wakutanisha wadau mbalimbali akiwemo mratibu wa mradi huo wa (BBT) Taifa kutoka wizara ya kilimo Vumilia L Zikankuba.

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo wa (BBT) Vivian Zikankuba amesema lengo la mradi huo ni kuwasaidia vijana katika kujiongezea ajira na kuondokana na umaskini na kuongeza dhamani katika masoko.

”Mradi huu unagusa vijana kulingana na vijana kutokana na  namna ambavyo wanaanza kujiwekeza katika shughuli hiyo ya kilimo lakini lengo letu kufikia mwaka 2030 tuwe tumezalisha ajira zaidi ya milioni sita kwa vijana na wanawake katika Taifa hili”.Ameongeza Viviani.

Aidha Mkurugenzi wa Mfuko wa Pemebejeo Taifa (AGITF) amesema wao wapo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wakulima wadogo ili kuendeleza Kilimo hicho na waweze kuhimili na bei za pembejeo  huku mfuko huo ukihudumia hasa wakulima wa Tanzania bara.

Nao baadhi ya vijana walio hudhulia katika mkutano huo wamesema licha ya changamoto zinazo wakabili kama masoko ya bidhaa ambazo wanazizalisha wamesema ni sehemu ya wao kwenda kubadirisha maisha yao katika kujitengenezea ajira pamoja na kuondokana na umaskini.

Please follow and like us:
Pin Share