Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati nchini Dkt ,Dotto Biteko ameshuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa mradi wa Uzalishaji umeme wa megawatt 49.5 kwa nguvu ya maji katika mto Malagalasi Mkoani Kigoma Utakaogharimu Dola za Kimarekani 144.14 na utachukua miezi 42 hadi kukamilika.
Amesema Serikali imeamua kutekeleza miradi mipya ya uzalishaji wa umeme badala ya kutegemea vyanzo vya zamani ili kuendana na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme nchini.
mradi huo ambao utatekelezwa na wakandarasi wa Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation ya Nchini China utasaidia kuvijenga vyanzo vya Umeme nchini ili kuweza kukabiliana na Upungufu wa Umeme ambalo limekuwa ni mwiba kwa Taifa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo jana jijini hapa amesema nchi ya Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa wa Nishati ya Umeme na mahitaji hayo yamekuwa yakuongezeka kila siku huku vyanzo vikibaki kuwa vile vile hali hiyo imekuwa ikipekekea Upungufu katika Vyanzo vya Umeme.
Amesema kutokana na mahitaji ya umeme kuwa makubwa kuliko vyanzo vyake, Serikali inaendelea kuongeza vyanzo vipya ikiwemo mradi wa Malagarasi ambao utekelezaji wake utachukua miezi 42 na utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimia 96 na unatarajia kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa mwezi huu.
Alisema, “Kunahaja kubwa ya kuhakikisha tunaongeza Vyanzo vingine na kwanza kujengwa kuanzia sasa ili tuweze kupata Umeme wa kutasha nchini na kuu za Umeme nchi jirani, miradi inahitaji muda wa kuwekeza na kuitunza lakini pia Serikali inaweka msukumo mkubwa kuhakikisha suala la Nishati sio tatizo ndani ya nchi, “alisema.
Akizungumzia hali ya umeme Mkoani Kigoma, Dkt. Biteko amesema Pamoja na mradi wa Mto Malagarasi, kuna miradi mingine mitatu ikiwemo usafirishaji wa umeme kutoka Nyakanazi hadi Kigoma (kV 400), Tabora hadi Kigoma (kV 132), kuongezwa uwezo wa kituo cha umeme wa Jua cha Kigoma kutoka megawati 5 hadi megawati .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu shirika la Umeme Tanesko Mhandisi Gissima Nyamuhonga amesema ujenzi wa mradi huo Utagharimu Dola za Kimarekani 144.14 na utachukua miezi 42 hadi kumalizika .
Pia ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa mkopo nafuu kwa kutoa Dolla za kimarekani Milioni 140 huku Serikali ya Tanzania kutia Dolla Million 4.4.
Amesema mradi wa kufufua Umeme kwa nguvu ya maji wa Mto Malagalasi upo kilometa 100 kusini mwa Mji wa kigoma, kilometa 27 kusini mwa Barabara kuu ya Uvinza – Kigoma katika Kara ya Kazuramimba kijiji cha Igamba kwenye Mto Malagalasi wenye lengo kuu la kuboresha usambazaji wa Umeme Magharibi mwa Tanzania ili kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi katika mikoa ya Magharibi mwa nchi ikiwemo kigoma.
Mradi huo utawezesha ongezeko la Umeme katika Gridi ya Taifa na kuwezesha biashara Umeme wa kanda na mradi wa Malagalasi unatarajiwa kuzalisha Umeme wa wastani wa Gigawati 181 kwa mwaka .
Lakini pia amesema mradi kabla ya kuanza ulikuwa na changamoto ya kumpata mkandarasi na tatizo hilo liliweza kupatiwa ufumbuzi
Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, amesema mradi huo wa Mto Malagalasi ni miongoni mwa Miradi ambayo ilianza kwa muda mrefu ambapo Serikali ilikuwa imeagiza mikoa ambayo haijaunganishwa na Gridi ya Taifa iunganishwe kwa haraka ili kuharakisha maendeleo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema maono na maelekezo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu uzalishaji wa nishati mkoani humo yameuheshimisha Mkoa wa Kigoma na Taifa kwa ujumla.
Amesema uzalishaji wa megawati 49.5 za umeme utapunguza gharama za uendeshaji ambapo kwa sasa zinatumika lita 28,000 za mafuta kwa siku kwa ajili ya kuzalisha umeme
Hafra hiyo ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Gridi ya Uzalishaji wa Umeme wa Megawati 49.5 kwa nguvu ya maji ya Mto Malagarasi, umesainiwa Kati ya Tanesco na Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation ya Nchini China.