Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mtwara

Mtandao wa Bayoanuai Tanzania umeomba serikali kufanya mabadiliko kwenye  sheria ya Mbegu ya Mwaka 2003 na mabadiliko yake madogo ya Mwaka 2012 ili kuipa nafasi mbegu ya asili ya mkulima kutambulika na kuingizwa sokoni kama ilivyo kwenye mbegu za kisasa.

Akizungumza na wanahabari katika  zoezi la utafiti shirikishi wa mbegu za asili za zao la ulezi Mkoani Mtwara,Mtaalamu wa Utafiti wa Masuala ya Sera kutoka mtandao huo, David Manogi amesema  mabadiliko hayo yatahakikisha wakulima  wananufaika moja kwa moja na  mbegu za asili ambazo zinapatikana kutoka kwenye maeneo yao.

Utafiti huo umeandaliwa na Mtandao wa Bayoanuai Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) Kituo cha Maendelea chini ya  ufadhili wa Shirika la SWISSAID Tanzania.

“Tunaomba serikali itambue mabadiliko haya na pia iweke kwenye mpango mkakati kuhakikisha kwamba wakulima wananufaika moja kwa moja na nasaba za mimea ambazo ni mimea asilia inayopatikana kutoka kwa maeneo ya wakulima,” amesema

Please follow and like us:
Pin Share