Mkurugenzi wa Ranchi ya Mbogo Pirmohamed Mulla (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb) nyaraka ya umiliki wa ng’ombe dume aina ya boran kwa serikali, baada ya ranchi hiyo kutoa msaada kwa serikali ili ng’ombe huyo atumike kuzalisha mbegu na kupandikizwa kwa ng’ombe jike ili kuboresha mifugo nchini. Makabidhiano hayo yamefanyia katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya.Picha zote na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Mb) akimfanyia tathmini ng’ombe dume aina ya boran mwenye umri wa miaka mitatu ambaye ana kilogramu 624 na ana thamani ya Shilingi Milioni Sita baada ya serikali kukabidhiwa ng’ombe huyo kutoka Ranchi ya Mbogo, ambapo Waziri Ndaki amesema dhamira ya serikali ni kuhimilisha ng’ombe jike Laki tatu kwa mwaka wa fedha 2022/23, hivyo ng’ombe huyo atapelekwa katika Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji kilichopo jijini Arusha kwa ajili ya kuzalisha mbegu. Waziri Ndaki amebainisha hayo baada ya makabidhiano ya ng’ombe huyo yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale yanapofanyika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) kitaifa jijini Mbeya.