Na Cresensia Kapinga,JamhuriMedia, Mbinga

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imejipanga katika kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi kwa kuhakikisha kuwa huduma za umeme zinaenda vizuri kama zilivyopangwa na kupeleka magari ya kubebea nguzo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Mbinga .

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati alipokuwa akizindua gari la kubebea nguzo za umeme Wilayani Mbinga ambapo amesema wamekuwa na utaratibu wa kutoa magari ambayo yamekuwa yakisaidia utekelezaji wa shughuli Mbalimbali ambazo zinzleta tija kwa wananchi ambao ni wateja wa shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwa kwenye gari ya kubebea nguzo ya shirika la umeme Tanzania (Tanesco)ambayo ameikabidhi Jana kwenye ofisi za shirika hilo Wilayani Mbinga.

Naibu Waziri kapinga ambaye pia ni Mbunge wa viti Maalumu kupitia Vijana Taifa amewahahkikishia Wananchi chini ya uongozi wa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassani na wasaidizi wake wanajitahidi katika kuhakikisha matatizo yanayo wakabili wananchi yakiwemo ya umeme yanapatiwa utatuzi wa haraka ndio maana kwa hivi sasa yameletwa magari maalumu kwaajili ya kubebea nguzo ambazo zinapaswa kusambazwa kwenye maeneo ya Mijini na Vijijini ambako huduma za umeme zinahitajika.

‘gari hili lililo zinduliwa leo ni moja kati ya magari yaliyoletwa na Shirika la Umeme(Tanesco) na yamegawanywa katika Wilaya Mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Mbinga ambayo bado inatatizo la upatikanaji wa Umeme na magari hayo ni kwaajili ya kubebea nguzo kutoka eneo moja kwenda eneo nyingine na Tanesco wataendelea kuboresha mazingira ya kazi ya kuhakikisha umeme unafika kwenye vijiji,,alisema Naibu Waziri.

Naibu Waziri Kapinga aliwataka kuona umuhimu wa kuyatunza magari ambayo yamepelekwa kwenye Wilaya Mbalimbali hapa Nchini kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma za umeme kwa wateja na amewahakikishia wananchi kwamba chini ya uongozi wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko watajitahidi kwa kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali ikiwemo namna ya kusambaza nguzo kutoka eneo moja kwenda eneo nyingine zinatatuliwa.

Alisema kuwa kwa hivi sasashirika la umeme (Tanesco) pamoja na Wizara ya Nishati wapo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Wilaya ya Mbinga ili kupunguza matatizo ya kukatika umeme kutokana na laini ya umeme kuwa ndefu kutoka Songea kwenda Mbinga ipo katika hatua ya utekelezaji na kwamba upo mpango wa utekelezaji Zaidi na kituo hicho kwa awamu ya pili kipo kwenye utekelezaji.

Alieleza Zaidi kuwa analishukuru Shirika la Umeme Tanzania kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambapo hadi hivi sasa wamepita kuboresha Zaidi miundombinu ya umeme ili kupunguza changamoto ya kuto kukatika umeme.

Mapema akizungumzia juu ya hali ya umeme Wilaya ya Mbinga Mhandisi Edward Kweka alisema Tanesco ilishaanza kuboresha na kukarabati miundombinu ya kusambaza umeme ili wateja waweze kupata umeme wa uhakika na wakuaminika na si vinginevyo na kwamba wateja waweze kupata huduma iliyo bora kwani wanatarajia kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kufungua ofisi ndogo katika maeneo madogomadogo ndani ya Wilaya ya Mbinga.