Serikali imesema kuwa kuna mambo matatu yaliyosababisha mfumuko wa beo na kupanda kwa gharama za bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi.
Hayo yamebainishhwa leo Juni 15, 2023 na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba,wakati akiwasilisha bungeni hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024,mkoani Dodoma.
Mwigulu amesema kuwa miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni kupanda kwa gharama za bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi kama petroli, mafuta ya kula, mbolea, ngano na malighafi za viwandani ambapo kutokana na umuhimu zimegusa maisha ya kila siku athari na kuleta athari.
Pia kupungua kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya masoko ya ndani kulikosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, hususan katika maeneo yanayotegemea mvua za vuli kwa ajili ya kilimo.
Waziri amesema kuwa mwaka 2022 mfumko wa bei ulikuwa ni asilimia 4.3 ukiongezeka kutoka wastani wa asilimia 3.7 mwaka 2021 ambapo kiwango cha sasa cha mfumko wa bei kipo ndani ya lengo la nchi la muda wa kati na kinakidhi vigezo vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) (asilimia 8) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) (asilimia 3 hadi 7).
Hata hivyo ameongeza kuwa sababu nyingine ni changamoto za athari ya mabadiliko ya tabianchi na pia vita inayoendelea nchini Ukraine.