Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi mfano wa funguo kwa familia ya John Mwangosi wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba na maeneo ya biashara kwenye mradi wa Morocco Square unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 1 Julai 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi mfano wa funguo kwa Bi. Aisia Mushi wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba na maeneo ya biashara kwenye mradi wa Morocco Square unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 1 Julai 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Hamad Abdallah wakiwa wameshikilia mfano wa funguo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba na maeneo ya biashara kwenye mradi wa Morocco Square unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 1 Julai 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Hamad Abdallah wakiwa katika picha na wawakilishi wa wanunuzi na wapangaji wa nyumba za mradi wa Morocco Square wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba na maeneo ya biashara kwenye mradi HUO unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 1 Julai 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha kifaa kwa ajili ya tahadhari ya moto kwenye moja ya vyumba na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Hamad Abdallah wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba na maeneo ya biashara kwenye mradi wa Morocco Square unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 1 Julai 2023.

Sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi nyumba na maeneo ya biashara kwenye mradi wa Morocco Square unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 1 Julai 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) 

Na Munir Shemweta, WANMM

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaandaa sera itakayowezesha Diaspora kuwekeza katika ujenzi na kununua nyumba zitakazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa na waendelezaji wengine.

Hatua hiyo ni muendelezo wa azma ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ya kufungua milango ya uwekezaji kwa kutoa fursa kwa waekezaji mbalimbali.

Hayo yamebainishwa tarehe 1 Julai 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kuabidhi nyumba 43 pamoja na maeneo 49 ya biashara kwenye Mradi wa Morocco Square unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Alisema, mwaka jana Shirika la Nyumba la Taifa ilizindua sera ya ubia ya Shirika la Nyumba la Taifa ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kujenga majengo mapya kwenye viwanja au majengo ya shirika yaliyopo katikati ya miji yaliyopitwa na wakati.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, sera hiyo ya ubia ni muendelezo wa azma ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan ya kufungua milango ya uwekezaji kwa kutoa fursa kwa waekezaji mbalimbali.

Ametoa wito kwa watanzania waishio ughaibuni kutumia fursa ya sera ya ubia ya NHC iliyoboreshwa kuja kuwekeza katika sekta ya nyumba.‘’Uwekezaji huu uwe ni wa nchi nzima na siyo Dar es Salaam pekee kwa kuwa NHC inayo viwanja na majengo yaliyopitwa na wakati katika miji yetu mbalimbali nchini’’. Alisema Dkt Mabula

Akielezea zaidi kuhusu Mradi wa Morocco Square, Dkt Mabula alisema mradi huo ni kielelezo cha uboreshaji wa miji kwa kuondoa majengo machakavu na yaliyopitwa na wakati na kujenga majengo makubwa ya kisasa.

‘’Kwa dhati kabisa nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuukwamua mradi huu na kuwezesha kukamilika kwa majengo ya mradi huu wa Morocco Square’’ alisema Dkt Mabula

Alibainisha kuwa, ujenzi wa mradi huo una faida kubwa kwa kuwa unaongeza ajira, umeongeza pato la serikali kupitia kodi mbalimbali kama vile kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kodi ya ardhi na kodi ya majengo sambamba na kupendezesha mandhari ya miji.

Akigeukia suala la ununuzi wa nyumba za mradi huo, Dkt Mabula ameshauri taratibu za kupata hati pacha za umiliki (Unit title) ufanyike mapema kwa kuwa ndiyo salama ya milki pamoja na uwezesho katika shughuli za maendeleo.

Ametoa rai kwa wapangaji kutunza miundombinu katika jengo hilo ili kuendelea kulinda umaridadi wa uwekezaji uliopo katika viunga vya morocco square.

Hata hivyo, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukamilisha haraka taratibu zote baada ya hatua za ujenzi kukamilika ili wahusika wapate fursa ya kutumia hati zao kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kupata mikopo benki.

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdalah amesema, walionunua na kupangisha nyumba katika mradi wa Morocco Square wako katika maisha tofauti kwa kuwa mradi huo ni ghali kuliko kuliko miradi yote inayotekelezwa na shirika lake kutokana na kuwa na vifaa vyenye ubora wa hali ya juu,

‘’Tuko katika mradi wa kipekee na wanunuzi na hata wapangaji hawawezi kujutia kupanga ama kununua nyumba katika majengo haya ya Morocco Square.

Mmoja wa wateja wa NHC Abouubakar Aboubakar ameishukuru serikali pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuweza kufanikisha mradi huo na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.

‘’Ni wajibu wa sisi wananchi kushirikiana na serikali kwa kwenda pamoja ili tupate maendeleo na NHC imekuwa wasikivu na nimeridhika na kazi inayofanywa na shirika hilo’’ alisema Aboubakar.