Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema katika kuhakikisha uchumi jumuishi unafikiwa kwa watanzania wengi Serikali imedhamiria kuziunganisha wilaya zote nchini na makao makuu ya mikoa kwa barabara za lami.

Amesema hayo mjini Haydom wakati akishuhudia utiaji saini wa ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom KM 25 ambayo ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Naibu Waziri Kasekenya amebainisha kuwa nia ya serikali ni kuboresha mtandao wa barabara za uhakika na hivyo kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi.

Barabara ya Labay-Haydom km 25 ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha mikoa ya arusha-manyara-singida na simiyu hivyo kukamilika kwake kutaunganisha kwa urahisi mikoa ya kanda ya kaskazini na ile ya kanda ya ziwa na hivyo kurahisisha shughuli za usafiri.

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya, akizungumza na wananchi wa Haydom (Hawapo Pichani), mara baada ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Labay-Haydom km 25, Mkoani Manyara.

amesema Naibu Waziri Kasekenya. Mtendaji Mkuu wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila amesema mradi huo unatekelezwa kwa utaratibu wa sanifu na kujenga ili kurahisisha utekelezaji wake.

Amesema zaidi ya shilingi bilioni 42 zitatumika katika ujenzi wa sehemu ya Labay-Haydom KM 25 na Mkandarasi JIANGXI GEO-ENGINEERING GROUP Limited kutoka China ndiye aliyeshinda zabuni hiyo na ujenzi utatumia miezi 18.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila, akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya (Hayupo pichani), katika hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom km 25, Mkoani Manyara.
Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya dola na Wananchi wa mkoa wa Manyara, wakishuhudia utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom km 25, Mkoani Manyara.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Rogatus Mativila na Mwakilishi wa kampuni ya Mkandarasi JIANGXI GEO-ENGINEERING GROUP Limited kutoka China wakisaini mikataba wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Labay-Haydom km 25, Mkoani Manyara.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI.