Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Serikali kupitia Mamlaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema itatoa ushirikiano na Chama cha Wafanyabiashara wa Gesi ya Kupikia Majumbani kwenye Nishati Safi Endelevu (TZLPGA) kimesema kitahakikisha ifikapo mwaka 2033 Watanzania asilimia 80 wataachana na matumizi ya nishati chafu ikiwemo mkaa na kuni na wanatumia nishati safi ya gesi ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira .
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk James Andililewa, amesema chama cha LPGA ni wadau muhimu kwa serikali kwani uwepo wake itasaidia kufikia ndoto ya Serikali kusaidia wanaichi kuachana na matumizi ya mkaa na kuni kwani kuna madhara makubwa hivyo chama hicho hakina budi wasogeze huduma karibu na wananchi kwani station 37 zilizopo nchi nzima hazitoshi waliangalie hilo kwa jicho la tatu
” Niwapongeze chama hiki kwa juhudi kwani takwimu zinaonyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la watumiaji nishati mbadala ampapo mwaka 2020 uagizaji ulikuwa tani milioni 20 tu mpaka mwishoni mwa mwaka 2023 tani laki mbili na tisini na tatu zimeagizwa hivyo pia watoa huduma wa LPG hivyo ni fursa kwa Serikali kupatikana kwa ajira na upatikanaji wa mapato” amesema Mkurugenzi.
Aidha amesema EWURA itakuwa inasimamia usalama wa utoaji wa huduma kwani mpaka mwaka 2023 tumeshatoa leseni kwa makampuni 11 na wasambazaji 101na leseni za.wauzaji rejareja 2000 kwani ni soko linalokuwa hivyo lazima lisimamiwe vizuri soko hilo lisije likaleta madhara
Kwa upande wake Mkurugenzi waa chama hicho (TZLPGA), Amosi Mwansumbue amesema watahakikisha bei inakuwa rafiki kwa wananchi kwani walio wengi wanaishi vijijini na vipato vyao ni vya chini hivyo wamekuwa wakiangalia jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kusaidia utunzaji wa mazingira kwa kununua mitungi ya gesi kuisambaza kwa wananchi wake bure ili nao waachane na matumizi ya nishati chafu .
Pia amebainiasha chama hicho kimeanzishwa mwaka 2023 kikiwa na wanachama Kampuni 6 wanaoingiza na kusambaza gesi LPGA wakiwa na lengo la kusaidia kuunganisha nguvu ya sauti moja kusaidia kutatua changamoto zinazowakumba ikiwemo kupatikana wataalamu wa ufundi pia usalama wa gesi kwani kumekuwa na watu ambao siyo waadilifu wanaharibu soko kwa kutumia baadhi ya mitungi ya gesi kujaza gesi na kusambaza hivyo malalamikiwa kwa watumiaji kusema mitungi inaisha haraka .
” Katika kipindi cha mwaka mmoja tulionza kutokana na changamoto ya kukosa wataalamu wa kufunga gesi tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pia ili kusaidia kupata wataalamu wengi kadri chama kinavyendelea kufanya kazi zake za kuhakikisha hakuna uhaba wa gesi nchini” amesema mkurugenzi.
Kwa upande wake Mwenyenyekiti wa Chama hicho, Bertnoit Araman amesema bei ya gesi inategemeana na nkoa husika kwani hivyo wananchi wasilalamike sana kwani kuna usafiri pia Watahakikisha wanashirikiana na serikali ili wananchi waachane kabisa na utumiaji nishati chafu hali inayosababisha mazingira kuharibika na kusababisha majanga ikiwemo ukosefu wa mvua .