Serikali imesema ina mpangokazi wa kupandisha thamani ya soko la madini ya tanzanite kwenye soko la dunia.

Waziri wa Madini, Antony Mavunde amesema hayo wakati akihutubia wafanyabiashara wa tanzanite, wamiliki wa migodi ya madini hayo, wachimbaji na wauzaji.

Mkutano huo wa hadhara ulifanyika ndani ya ukuta wa madini ya tanzanite katika mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara.

Mavunde amesema baada ya kuona thamani ya madini ya vito inashuka waliunda kamati ya wataalamu kutoka Wizara ya Madini wafanye utafiti wa ndani ya nchi na nje na watoe majibu ya kuboresha biashara ya tanzanite.

Aliongeza kuwa, kamati hiyo ilipendekeza kubadilisha sheria ya madini ya tanzanite kwa maslahi ya nchi.

Mavunde amesema  soko la madini ya tanzanite litabaki katika mji wa mirerani na kwamba madini hayo yataongezewa thamani ndani ya ukuta wa mirerani kama Rais Samia Suluhu Hassan na Wa ziri Mkuu, Kassim Majaliwa walivyoagiza.

Alisema ujenzi wa jengo la Tanzanite City katika mji wa Mirerani unaogharimu zaidi ya Sh bilioni tano umefikia asilimia 80 na wiki ijayo mkandarasi anakabidhiwa fedha amalizie kazi.

“Jengo la Tanzanite City ni la kimataifa hivyo eneo hilo linapaswa kuwa la kimataifa na Halmashauri ya Siman jiro inapaswa kuwajibika kwa hilo ikiwa ni pamoja na kupanda miti eneo husika ili kuwa na mandhari nzuri ya kuvutia,” alisema Mavunde.

Please follow and like us:
Pin Share