Na Rahma Khamisi Maelezo
Waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi Dkt Khalid Salum Muhammed amesema Serikali inatambua michango ya Viongozi walioshiriki katika kuikomboa nchi ambao wameshatangulia mbele ya haki.
Ameyasema hayo huko Migombani Wilaya ya Mjini katika dua ya kumuombea aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi.
Amesema Serikali imeweka utaratibu wa kuwaombea dua wazee hao kwa madhumuni ya kuwaenzi kwani wamefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo nchini.
Aidha amefahamisha kuwa kufanya hivyo ni kufuata mwenendo wa Mtume Muhammad SAW kwa vile yeye ndio kigezo cha waumini.
“Hatuna budi kuwaenzi mwaka hadi mwaka kwani utaratibu wa kuwaombea dua waliotangulia ulikua unafanywa na Mtume wetu Muhammad (SAW) na sisi hatuna budi kuyafanya,”” alifahamisha Dkt Khalid.
Ameongeza kuwa Mtume Muhammad ( S .A W) alisema kuwa mwanadamu atakapomaliza uhai wake mambo matatu ndio yatabaki ikiwemo kutoa sadaka inayoendelea, kuacha mtoto mwema mwenye kumuombea dua na elimu yenye manufaa hivyo kuendeleza dua hizo ni jambo jema.
Aidha amewashukuru wanafamilia kwa ushirikiano wao mzuri kwani kila mwaka wamekua wakishirikiana katika kufanikisha suala hilo.
Akitoa shukurani kwa niaba ya familia Shekh Mustafa ameishukuru Serikali kwa utaratibu huo kwani wanafarijika kuona Serikali inathamini juhudi za wazazi wao.
Wiki ya kuwakumbuka na kuwaenzi viongozi waasisi huanza kila ifikapo April mosi na kufikia kilele chake April saba ambapo viongozi wa serikali, dini , vyama pamoja na wananchi hujumuika pamoja kumuombea dua aliyekuwa rais wa awamu ya kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume huko Kisiwandui Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohammed akiwaongoza wananchi na familia katika dua ya kumuombea aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya pili marehemu Aboud Jumbe Mwinyi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya kuwakumbuka viongozi wa Kitaifa inayoanzia April 1-7 huko Migombani Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe.Rashid Simai Msaraka akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na uchukuzi Dkt.Khalid Salum Mohammed kuzungumza na familia mara baada ya kumuombea dua aliekua Rais wa awamu ya pili marehemu Aboud Jumbe Mwinyi katika wiki ya kuwakumbuka viongozi wa Kitaifa inayoanzia April 1-7 huko Migombani Zanzi