Mkurugenzi wa Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza wakati akifungua Mkutano
wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii kwaniaba ya waziri wa wizara hiyo. Mkutano
huo uliandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation kwa kushirikiana na asasi ya
An Nahl Trust.

Mkurugenzi wa Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai (kulia) akizungumza wakati akifungua Mkutano
wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii kwaniaba ya waziri wa wizara hiyo. Mkutano
huo uliandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation kwa kushirikiana na asasi ya
An Nahl Trust.

Mwenyekiti wa Asasi ya An Nahl Trust, Mhandisi Alliy
Kilima akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii
nchini Tanzania ulioandaliwa na asasi yake kwa kushirikiana na NAMA Foundation leo
jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa
Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa
ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar
es Salaam.

Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa
Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa
ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar
es Salaam
 
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa
Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa
ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar
es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa asasi ya An-Nahl Trust, akizungumza katika mkutano huo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

SERIKALI inatambua na kuthamini juhudi za wadau mbali
mbali zinazofanywa zenye lengo la kuhakikisha maendeleo ya Watanzania yanawezeshwa
kikamilifu, hasa zinazochochewa na asasi za kiraia.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim katika hotuba yake iliyosomwa na
Mkurugenzi wa Watoto wa wizara hiyo, Margaret Mussai alipokuwa akifungua Mkutano
wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii ulioandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation.
Akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha asasi
mbalimbali za kiraia, alisema Serikali inafarijika kuona wadau wakiungana na
kupanga mikakati ya kufikia malengo ya mafanikio ya utendaji kwa pamoja
kuihudumia jamii.
“…Asasi za kiraia mmekuwa muhimili muhimu kwenye
kuhimiza maendeleo ya jamii, mmekuwa mnabuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha
vijana na wanawake kiuchumi na kutoa huduma za maendeleo ya Jamii kwa kutumia
gharama nafuu na hata muda mwingine kwa kutumia rasilimali za wanaojitolea,”
“…Tunatambua mchango wa asasi nyingi za kiraia
zinazotoa elimu juu ya mapambano ya magonjwa yanayoambukizwa, mila na desturi
zenye madhara kwa vijana wakiwemo watoto wa kike na wanawake. Lakini pia kuna
asasi zinazowezesha vijana kuwekeza kiuchumi katika miradi midogomidogo ya
uzalishaji mali,” alisema Ummy katika hotuba hiyo.
Aidha alisema licha ya Serikali kutambua mchango
mkubwa wa asasi za kijamii, alizitaka kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na
ushirikishwaji wa rika zote, huku zikizingatia sheria na katiba ya nchi ili
kufikia malengo yao.
Alizipongeza asasi
za
An Nahl
Trust pamoja na
NAMA
Foundation kwa kufanikisha mkutano huo uliowakutanisha kwa pamoja wadau
mbalimbali toka asasi za kiraia kuwajengea uwezo ukiwa na lengo la kuwajengea
uwezo katika shughuli wao.
Kwa pande wake
Mwenyekiti wa An Nahl Trust, Mhandisi Alliy Kilima alisema mkutano wa mwaka huu
umekuja na maudhui mapana zaidi kuliko ule wa mwaka jana na umedhamiria kutoa
taarifa kuhusu Maeneo yanayo lengwa na NAMA na Washirika wake ambayo ni
‘Kuwezesha sekta ya Elimu, Kuwezesha sekta ya asasi za kiraia na Kuwawezesha
vijana,’ Na uwezeshaji wenyewe ni ule ule katika kukuza vipaji, maarifa, stadi
na jinsi ya kuyaangalia mambo kwaupana wake.
Alisema mkutano
huo utakuwa na watoa mada wataalam wa masuala mbalimbali watakao wajengea uwezo
washiriki hususan katika mafunzo na idili za kujiendesha kwa kufuata taratibu
na misingi mwafaka katika asasi zao.
 
Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.