Serikali imesema ina matumaini makubwa na timu za Yanga na Simba katika michezo yao ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Ijumaa wiki hii.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma na kusema licha ya Simba kupoteza kwa bao 1-0 na Yanga kutoka 0-0 matumaini ya timu hizo kuingia Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ni makubwa.
Simba ilifungwa na Al Ahly, wakati Yanga ilitoka suluhu na Mamelodi katika michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Yanga itarudiana na Mamelodi Ijumaa nchini Afrika Kusini, ikihitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya idadi yoyote ya mabao itakuwa imefuzu hatua inayofuata, huku Simba yenyewe ikirudiana na Al Ahly nchini Misri na inatakiwa kushinda kuanzia mabao 2.