Naibu Waziri Ofisi ya Rais -TAMISEMI (Elimu),David Silinde amesema Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imadhamiria kwa dhati kuhakikisha inamaliza changamo zote za elimu Msingi nchini.
Ameeleza hayo tarehe 19 Februri 2023 wakati wa Mahafali ya tatu ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Ziba iliyopo Igunga mkoani Tabora.
Silinde amesema wakati Rais Dkt. Samia anaingia madarakani amekuta changamoto nyingi katika sekta ya elimu, ambapo mara baada ya kungia madarakani alitoa shilingi bilioni 300 kujenga madarasa mpya 15,000 nchi nzima.
“Vile vile Mwaka jana Mheshimiwa Rais,Dkt.Samia alitoa bilioni 160 kujenga madarasa 8,000 yaliyowawezesha wanafunzi wote waliomaliza shule ya msingi kuingia kuanza masomo ya kidato cha kwanza kwa wakati Mmoja mwezi Januari 2023” amesema Silinde
Aidha,Silinde amesema Serikali iliweka mkakati wa kujenga shule za sekondari katika Kata ambazo hazikuwa na shule hizo, ambapo zitajengwa Shule za Sekondari za Kata 1,000 nchi nzima.
“Awamu ya kwanza, mwaka jana tulijenga shule 234 na katika awamu ya pili muda wowote kuanzia wiki ijayo inatolewa fedha ya kujenga shule za kata nyingine 184” amesema Silinde.
Silinde amesema kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) zitajenjwa shule za Sekondari maalum katika mikoa yote 26 ambapo kila Shule itagharimu bilioni 4 na katika awamu ya kwanza tayari zimejengwa Shule 10.
Kadhalika, amesema kupitia Mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) utawezesha ukarabati shule za msingi zote chakavu na kujenga shule nyingine mpya za msingi.