Brett Kavanaugh, mteule wa Rais Donald Trump katika nafasi ya Mahakama ya Juu Marekani, Ijumaa alionekana kuwa anaelekea atapitishwa na Baraza la Seneti baada ya siku nne za mahojiano ambapo alifanikwa kujiepusha na vizingiti vikubwa pamoja na Wademokrati kujaribu kwa hasira zote kuzuia uteuzi huo.

Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnel, aliulizwa na mwendesha kipindi mkonservative Hugh Hewitt katika mahojiano na idhaa ya televisheni ya MSNBC iwapo alikuwa na mashaka yoyote juu ya kupitishwa kwa Kavanaugh, na kujibu: “Sina wasiwasi wa namna yoyote.”

McConnell alitabiri kuwa Kavanaugh, ambaye ni jaji wa mahakama ya rufaa ya serikali kuu mconservative aliyeteuliwa na Trump kwa ajili ya nafasi ya kazi katika mahakama ya ngazi ya juu Marekani kwa kipindi cha uhai wake wote, atakuwa katika Mahakama ya Juu wakati itakapoanza mhula wake mpya Octoba 1.

Wenzake Trump katika chama cha Republican ambao wana maamuzi kutokana na idadi yao kuwa juu kidogo kuliko Wademokrat katika Baraza la Seneti. Kukiwa hakuna dalili ya Mrepublikan kuwa ana mpango wa kupiga kura dhidi ya Kavanaugh, inaelekea kuwa atapitishwa kwa ushindi pamoja na Wademokrat kupinga hilo.

“Nafikiri ameweza kutoa hoja ya nguvu kuwa yeye ni mteule aliye na sifa zaidi kuchukua nafasi hiyo kati ya wateule wengine, na pengine ndiye mwenye sifa zaidi, ambaye tumewahi kumuona akiteuliwa katika Mahakama ya Juu ya Marekani, na nafikiri nimewahi kuwaona 15 kati ya hao,” amesema Mwenyekiti Mrepublikan wa Kamati ya Sheria Chuck Grassley, ambaye amesimamia mahojiano hayo na ametumikia Baraza la Seneti tangu mwaka 1981.

Kavanaugh alimaliza siku mbili za mahojiano marefu yaliyo fanywa na maseneta Alhamisi usiku, akiendelea kuwa mtulivu wakati akiulizwa maswali magumu na Wademokrat. Kavanaugh kuna uwezekano kuwa atakuwa atamili zaidi mrengo wa kulia wa majaji waconservative, iwapo atathibitishwa.

Katika siku yake ya mwisho ya mahojiano, kamati hiyo Ijumaa imesikiliza Ushahidi kutoka kwa mashuhuda ambao sio maseneta waliokuwa baadhi wanaunga mkono uteuzi wake na wengine kupinga kuteuliwa kwake, pamoja na kuwepo waandamanaji waliokuwa wakiingilia kati mahojiano hayo wakipinga uteuzi wa Kavanaugh.

Kati ya wale waliotoa Ushahidi ni wawakilishi wa chama cha Wanasheria wa Marekani, ambacho kinaongoza kundi la mawakili wanaofanya kazi hiyo, ambao wamesema kuwa jopo linalowapima wateule wa nafasi za sheria wamempa Kavanaugh sifa ya kuwa “anastahili ipasavyo” kushikilia nafasi hiyo.