Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Jeshi la Polisi limeeleza kuridhishwa na huduma bora inayotolewa na sekta binafsi ya ulinzi ambayo imesaidia kuendeleza usalama wa raia na mali zao hapa nchini.

Mkuu wa Ushirikishwaji Jamii wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni ASP Elina Maro ameeleza hayo wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wateja duniani, iliyoandaliwa na Kampuni Binafsi ya Ulinzi ya G4S ya jijini Dar es Salaam.

Ameipongeza kampuni hiyo kwa rekodi nzuri ya utoaji huduma bora kwa wateja raia wa Tanzania na wa kigeni wanaoishi nchini wakiwemo wawekezaji, na kuomba ufanis huo uendelea kwa faida ya vijana walioajiriwa lakni pia kwa usalama wa nchi.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa G4S Imelda Lutebinga alisema ufanisi wa kampuni hiyo iliyosambaa nchini kote na nje ya nchi unatokana na kupokea ushauri na maoni kama mrejesho wa huduma inayotolewa kwa wateja wake.

Miongoni mwa huduma za Kampuni hiyo ni ulinzi wa kawaida, usafirishaji wa fedha na huduma nyingine ambazo ni suluhisho kwenye mifumo mbalimbali ya kiusalama.

Please follow and like us:
Pin Share