Archives
Wakenya, NGOs wanavyoivuruga Loliondo
*Mkutano Mkuu wa Kata Oloipir watoa tamko
*Dk. Mary Nagu aandikiwa waraka maalumu
Magufuli amvimbia Pinda
Kuna kila dalili kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli, amekataa au kushindwa kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na kilichoelezwa kuwa kuyatekeleza ni kuvunja sheria ya usalama barabarani na kanuni zake, hivyo yeye hayuko tayari kufanya hivyo.
Pinda: Mwanasheria anayepinda sheria
Kuna mambo mengine mtu unaweza kupata sifa hata kama huna ujuzi nayo. Wakati wa mvutano wa Chama cha Wamiliki wa Malori na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, nilisema Waziri huyo hatafika mbali kwa uamuzi wake wa kusimamia sheria.
Malinzi: Tuelekeze nguvu Morocco vs Taifa Stars
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera, Jamal Malinzi, amewataka Watanzania kuiunga mkono Taifa Stars iweze kushinda katika mchezo kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia unaotarajiwa kufanyika Machi 24, mwaka huu.
Mashindano ya Miss Tanzania yafutwe
Wakati huu wa harakati za kutoa maoni ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wakati mwafaka kutafakari kama mashindano ya ‘Miss Tanzania’ yanaikosea Tanzania. Mwaka 1964 Serikali ilipiga marufuku mashindano hayo lakini yakaibuka kinyemela mwaka 1994 kwa mfano wa Azimio la Zanzibar, lililoibuka mwaka 1992 bila mwafaka wa kitaifa, na kuathiri Azimio la Arusha lililozaliwa mwaka 1967.
Vituo vya mafuta vinaiba kodi mchana kweupe
Mzee Ali Hassan Mwinyi alipata kusema maneno haya: “ Tanzania ni sawa na kichwa cha mwendawazimu.” Maneno haya aliyasema kwa maana kwamba kichwa cha mwendawazimu kila anayejifunza kunyoa hufanyia hapo mazoezi. Wiki iliyopita nilikuwa Nairobi , Kenya ambako nilikuwa na mafunzo ya wiki zaidi ya mbili. Nikiwa huko kwa mshangao nikakuta Tanzania inamwagiwa sifa.