RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kusafiri kwa treni ya reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma Agosti Mosi, mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano cha Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk amesema Rais Samia anatarajiwa kuzindua safari za treni ya SGR Agosti Mosi, mwaka huu jijini Dodoma.

Mbarouk amesema safari za treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma zinaanza leo lakini uzinduzi utafanyika Agosti Mosi Dodoma.

Kuhusu safari za treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro zilizoanza Juni 14, mwaka huu, alisema mpaka sasa hakuna changamoto za kiuendeshaji na safari zinaenda kama zilivyopangwa. Hivi karibuni, TRC ilitoa ratiba ya safari na kusema treni ya haraka itatoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na itatoka Dodoma saa 5:30 asubuhii.

Kwa upande wa treni ya kawaida itatoka Dodoma saa 11:30 jioni na itatoka Dar es Salaam saa 12:55 jioni.

Treni ya SGR ina vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambavyo ni Stesheni, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere, na Morogoro.

“Kwa treni ya kawaida inayoishia Morogoro itatoka Dar es Salaam saa 3:30 na kuwasili Morogoro saa 5:10, pia itatoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na kuwasili Dar es Salaam saa 5:40 asubuhi,” alisema Mbarouk.

Aidha, shirika limetoa masharti kwa abiria wasibebe mifuko ya plastiki, silaha, viroba,wanyama, ndoo au jaba, vinywaji au vyakula vya aina yoyote.

Abiria wanapaswa kubeba mizigo kulingana na daraja la tiketi. Daraja la biashara linaruhusu mzigo wenye uzito usiozidi kilogramu 30 na kwenye daraja la uchumi ni mzigo usiozidi kilogramu 20.

Abiria wenye tiketi wanapaswa kufika stesheni saa moja kabla ya kuanza safari na ambao hawana tiketi wafike saa mbili kabla ya safari.

Mkandarasi wa SGR, Yapi Merkezi amewataka wakazi wa Dodoma wachukue tahadhari kwa kutoikaribia au kukatisha reli ya umeme ya SGR na badala yake watumie vivuko vya juu na vya chini ni kwa wanyama.

“Tunasisitiza kuitunza miundombinu ya reli yetu ikiwemo kutokatiza fensi iliyowekwa pembezoni mwa reli kwa usalama wetu, mifugo na watoto hasa watoto wetu wa shule za msingi na sekondari,” ilieleza taarifa hiyo.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amehimiza wananchi wakiwamo waendesha bodaboda na bajaji kwenda kumpokea Rais Samia atakaposhuka katika kituo cha treni cha Mkonze akiwa amesafiri kwa treni hiyo kwa saa tatu.

Senyamule alisema hayo jana jijini Dodoma wakati akizindua ubandikaji mabango kwenye bajaji na bodaboda kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki maonesho ya wakulima (Nanenane) kikanda na kitaifa mkoani humo. Alisema Maonesho ya Nanenane kikanda yataanza Julai 31, yatafunguliwa Agosti Mosi na yatafungwa Agosti 9, mwaka huu.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano cha Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk amesema Rais Samia anatarajiwa kuzindua safari za treni ya SGR Agosti Mosi, mwaka huu jijini Dodoma.

Mbarouk amesema safari za treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma zinaanza leo lakini uzinduzi utafanyika Agosti Mosi Dodoma.

Kuhusu safari za treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro zilizoanza Juni 14, mwaka huu, alisema mpaka sasa hakuna changamoto za kiuendeshaji na safari zinaenda kama zilivyopangwa. Hivi karibuni, TRC ilitoa ratiba ya safari na kusema treni ya haraka itatoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na itatoka Dodoma saa 5:30 asubuhii.

Kwa upande wa treni ya kawaida itatoka Dodoma saa 11:30 jioni na itatoka Dar es Salaam saa 12:55 jioni.

Treni ya SGR ina vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambavyo ni Stesheni, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere, na Morogoro.

“Kwa treni ya kawaida inayoishia Morogoro itatoka Dar es Salaam saa 3:30 na kuwasili Morogoro saa 5:10, pia itatoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na kuwasili Dar es Salaam saa 5:40 asubuhi,” alisema .

Aidha, shirika limetoa masharti kwa abiria wasibebe mifuko ya plastiki, silaha, viroba,wanyama, ndoo au jaba, vinywaji au vyakula vya aina yoyote.

Abiria wanapaswa kubeba mizigo kulingana na daraja la tiketi. Daraja la biashara linaruhusu mzigo wenye uzito usiozidi kilogramu 30 na kwenye daraja la uchumi ni mzigo usiozidi kilogramu 20.

Abiria wenye tiketi wanapaswa kufika stesheni saa moja kabla ya kuanza safari na ambao hawana tiketi wafike saa mbili kabla ya safari.

Mkandarasi wa SGR, Yapi Merkezi amewataka wakazi wa Dodoma wachukue tahadhari kwa kutoikaribia au kukatisha reli ya umeme ya SGR na badala yake watumie vivuko vya juu na vya chini ni kwa wanyama.

“Tunasisitiza kuitunza miundombinu ya reli yetu ikiwemo kutokatiza fensi iliyowekwa pembezoni mwa reli kwa usalama wetu, mifugo na watoto hasa watoto wetu wa shule za msingi na sekondari,” ilieleza taarifa hiyo.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amehimiza wananchi wakiwamo waendesha bodaboda na bajaji kwenda kumpokea Rais Samia atakaposhuka katika kituo cha treni cha Mkonze akiwa amesafiri kwa treni hiyo kwa saa tatu.

Senyamule alisema hayo jana jijini Dodoma wakati akizindua ubandikaji mabango kwenye bajaji na bodaboda kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki maonesho ya wakulima (Nanenane) kikanda na kitaifa mkoani humo. Alisema Maonesho ya Nanenane kikanda yataanza Julai 31, yatafunguliwa Agosti Mosi na yatafungwa Agosti 9, mwaka huu.

Please follow and like us:
Pin Share