Na Cresensia Kapinga,JamhuriMedia, Songea

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan metoa miezi mitatu kwa wakala wa Maji Vijiji (RUWASA) kukamilisha mradi wa maji wa Mchangombole uliopo Halmashauri ya Madaba wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma na amewataka wananchi kutoharibu vyanzo vya maji kwani vyanzo hivyo ndio uhai wao kwa matumizi ya binadamu na wanyama.

Amesema kuwa miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali ili iweze kuwa endelevu ni pamoja na kuhakikisha miundombinu ya maji safi na usafi wa mazingira inalindwa kwakuwa maji ni rasilimali muhimu inayogusa maisha ya kila kiumbe.

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa vijiji vitatu uliopo katika Kijiji cha Mtyangimbole halmashauri ya Madaba ambao hadi kukamilika utakuwa umegharimu kiasi cha sh. Bilioni 5.5.

Amesema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kulinda chanzo cha maji cha mto Mtichi ambao upo katika hifadhi ya milima ya Matogoro B na sio jukumu la watu wa maji ambao kazi yao ni kuangalia maji yapo wapi ,watafanya nini ili maji yasambae yawafikie wananchi na si vinginevyo.

“Niwaombe kutoharibu kile chanzo Cha maji ule ndio uhai wenu,maji haya yatatumika kwa matumizi ya binadamu ,wanyama lakini pia kwenye baadhi ya maeneo , kwa hiyo niwaombe sana,sana msiende kuharibu kile chanzo kinachotupa maji kule mtoni tuende tutumie lakini kuwe na ulinzi wa kutosha ” amesema Rais Dkt. Samia.

Amesema kuwa katika Mkoa wa Ruvuma ameweka jiwe la msingi kwa miradi 30 inayoendelea mkoani humo, mradi huo utakwenda kuhudumia vijiji vitatu na ndio kusudio lakini kwa kuwa maji yatakuwa mengi yatakwenda kwenye Kijiji kwingine Cha nne .

“Ndugu zangu mnakumbuka wakati wa kampeni tuliahidi kumtua ndoo mama kichwani sasa tumeenda kuifanyia kazi habari ile tumeifanyia kazi kwa kusambaza maji Nchi nzima kama mnavyoona tulivyofanya hapa Ruvuma na hivyo hivyo kwa Nchi nzima kwa hiyo tunatarajia ikifika mwaka 2025 tuwe tumetimiza lengo la vijiji vyote vya Tanzania vipate maji” alisema Dkt. Samia.

Kwa upande wake katibu Mkuu Wizara ya maji Mwajuma Waziri akisoma taarifa ya mradi wa maji Mchangombole alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 50 na tayari Wamejenga inteki ambayo inauwezo wa kuzalisha maji Lita milioni moja na laki tisa na baada ya hapo watajenga mabomba yenye urefu wa mita 20.9 ambalo litafika kwenye matenki mawili yaliyojengwa hapo Mtyangimbole.

Ameongezs kuwa tenki moja linauwezo wa Lita 150 lipo kwenye leza ya mita sita na limeshakamilika na litahudumia wananchi wa Mtyangimbole ambapo watajenga vituo vya kuchotea maji 16 na watakua na mabomba ya usambazaji yenye urefu wa mita 11.9

Amesema,Tenki la pili linaujazo wa lita laki mbili litahudumia vijiji viwili kijiji cha Luhimba na Kijiji cha Likarangiro na watajenga mtandao wa maji wenye urefu wa km 19.97 na vituo 24 vya kuchotea maji hivyo kuwa na mtandao wa maji wenye urefu wa km 52.7 pamoja na vituo vya maji vipatavyo 40 ambapo mahitaji ya maji katika vijiji hivyo ni Lita 634 ambazo chanzo hicho kinauwezo wa kuzalisha lita 1.9 milioni hivyo Kuna maji yanabakia .

“Rais uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi huu unawakilisha miradi yote 30 ya maji inayoendelea kutekelezwa mkoani Ruvuma ambapo itakapokamilika itasaidia wananchi 14,000 kupata huduma ya maji safi na salama kwani hivi vijiji havijawai pata maji ya Bomba vinatumia maji ya visima vya zamani .”Alisema Waziri.

Naye Waziri wa Maji Juma Aweso amemshukuru Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kusema asoshukuru hato kwa Mungu hawezi kumshukuru, kwa dhati ya moyo sekta ya maji umewatoa mbali sana ambapo sekta hiyo ilikuwa kero na lawama kwa wananchi wameteseka kwa kiwango kikubwa sana,kutokana na adha ya maji.

“ulitupa maelekezo Wizara ya maji yapatikane maji miji na vijijini kwa sasa nakuhakikishia asilimia kubwa wanaoteseka juu ya adha ya maji ni akina mama,sitaki kusiikia sitaki kuona wamama wa Nchi hii wanateseka juu ya kukosa maji ,kazi umeifanya kwa muda mfupi inaonekana kwa macho, umetutoa asilimia 50 ya upatikanaji wa maji vijijini hadi asilimia 79 na tunamiradi zaidi ya 200 inayoendelea haijawahi kutokea sawa na asilimia 89, kwa mijini tupo zaidi ya asilimia 90 ya miradi inayoendelea na ikikamilika tutafika zaidi ya asilimia 95.” amesema Waziri wa Maji .

Amesema kuwa wamefanya tathimini Nchi yetu inavijiji 12318 kupitia wakala wa maji vijijini Ruwasa tumeshakwenda vijiji elfu 10 bado vijiji 2000,Tulikwama fedha tulizokuwa nazo kwenye miradi Tumepata zaidi ya sh. Bilioni 53 na mitambo umetupa tukasema tuweke hii awamu ya kwanza visima 900 mkakati wetu vijiji vyote vipatikane maji na Nchi hii tutailowanisha maji hatutaki kuwa kikwazo kwa wananchi.

Naye Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amemshukuru Raisi kwa kuendelea kutatua changamoto zao, kwa nafasi ya kwanza kabisa wananchi wa Madaba ,pamoja na viongozi wenzangu tunakushukuru sana katika kipindi chako Cha Uongozi katika Jimbo la Madaba tumepokea fedha za maendeleo bilioni 31.3 ambazo zinajenga miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yetu.

Amesema kuwa wanamadaba wanasema asante sana na kushukuru ni kuomba tena kwenye eneo la maji wamepokea bilioni 7.8 zinajenga miradi maeneo mbalimbali lakini wanachangamoto tunaomba tuongezee nguvu kwenye eneo la wino Kijiji Cha lilondo bado hapajakaa sawa sawa lakini miradi hii ambayo umeiona leo vijiji vyote vya Madaba tutakuwa tumefikiwa na maji.

“Katika sekta ya Afya mpaka Jana tumepokea vifaa tiba vya milioni mia 7.87 ambavyo tayari vipo kwenye hospital na tunaamini ukishamaliza ziara yako wananchi hawa watapata huduma za Afya bora kwenye hospital bora ambazo uezijenga wewe Rais wetu.” amesema.

Miradi ya umeme vijiji vyetu vyote vya Madaba vitakapofikia mwishoni mwa September Kila Kijiji kitakuwa kimefikiwa na umeme japo tulibakiwa na Kijiji kimoja kipo kilomita 48 kipo ifinga lakini kazi zinavyoendelea tutakuwa tumefikiwa ombi letu tutilie nguvu kwenye maeneo ya ambayo tunajaziliza umeme bado yanachangamoto za hapa na pale lakini kwa Kasi hii na kwa uwepo wako changamoto zote zitaishaa

Please follow and like us:
Pin Share