Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Mbinga
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na ujenzi wa Jengo la kisasa la ghorofa moja la Halmashauri ya wilaya ya Mbinga ambalo limejengwa kwa shilingi bilioni 3.3 hadi kukamilika kwake.
Alisema kuwa anawashukuru amefika Mbinga kwa madhumuni ya kufungua jengo na amewapongeza halmashauri hiyo kwa kukamilisha ujenzi huu wa jengo hilo zuri .
Akizundua jengo hilo Septemba 25/2025 amesema kukamilika kwa jengo hilo ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukamilika jengo hilo wahakikishie huduma zote zinatolewa ndani ya nyumba moja .
“Ni jengo zuri nimeingia ndani kuangalia ujenzi unaridhisha sana na ni jengo lenye nafasi za kutosha kwa hiyo nawashukuru sana lakini pamoja na hilo niwapongeze madiwani kwamba mmesimamia ujenzi wa jengo hili lakini pia mmewaza kuwa na jengo la kitega uchumi jengo la kuwawezesha wananchi nimuombe Mungu awatie nguvu na mlimalize jengo hilo liweze kufanya kazi iliyokusudiwa” alisema Rais Samia.
Alisema kuwa kukamilika kwa jengo hilo ni kukuwa kwa utawala bora maofisi yote wakiwemo wakuu wa idara na kila mtu yumo humo ndani kwa maana hiyo huduma zote zitatolewa ndani ya nyumba moja ili kuharakisha huduma kwa wananchi lakini pia kuleta utawala bora ili haki za wananchi zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo .
” Niwasisitize watakaotumia nyumba hii madhumuni ya serikali kujenga nyumba hizi ni kuleta mazingira mazuri kwa maafisa wetu wanafanya kazi ndani ya halmashauri hizi ni kurahisisha utendaji wa kazi kwa hiyo niwaombe sana maofisa wote kutumika Majengo haya kwa kutulia na kufanya kazi zao vizuri kwa kuhudumia wanachi kwa upendo na weledizaidi.”alisema Rais Samia.
Naye Mbunge jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga amesema,Wanamshukuru kwa miradi mingi aliyopeleka kwenye jimbo hilo wamepata miradi ya maji bilioni 13.9 , Barabara-Amani Makolo-Mbambabay bilioni 60 elimu bilioni 10 afya bilioni 2.2 ujenzi wa vituo vya Afya bilioni 836 na bilioni 2.8 upande wa Barabara.
Alisema kuwa pamoja na fedha zote za miradi yote ya maendeleo waliyopata anakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Mji huo wa Kiamili unakua kwa kasi jambo ambalo linasababisha huduma ya maji hayatosherezi.
Madini ya makaa ya Mawe wananchi hawakunufaika ila sasa wameanza kupata CSR ila bado wanamang’uniko makampuni yanapata pesa nyingi kuliko CSR inayopelekwa.Kahawa bila Ruzuku ya mbolea hawavuni .Changamoto ipo bado hawana maghala ya kuhifadhi mazao yao ila bado Kuna msululu mkubwa mtaaani 350 kwa kilo .
Kahawa haijauzwa chini ya 4000 mwaka huu kilo imeuzwa 10,000 hadi 12,000 kwa kilo .
Barabara amani Makoto hadi Ruanda desemba 18 , 2023 ila bado haujakamilika hadi leo kipande cha kwanza km 35 bado hakijakamilika wala kipande cha pili km 56 hakijakamilika.
Naye Mbunge wa Viti maalum kupitia vijana Judith Kapinga na Naibu Waziri Nishati amemshukuru Rais Samia Suluhu na amemuomba awasaidie kuweka kituo cha Zana za kilimo ili wakulima waweze kuzalisha kwa wingi mazao yao.
Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengelwa amemshukuru Rais kwa kuwajengea Jengo zuri lililogharimu sh 3.3 bilioni wananchi hivyo kusogeza huduma kwa wananchi kwani wameteseka kwa muda mrefu kutafuta huduma za kijamii, ametoa sh 500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule tatu za kata fedha zifike mara moja kujenga shule hizo.
Naye Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema kuwa Bilioni 10 zimeshalipwa kwa wakulima kuanzia mwaka kesho vituo vyote vya NFRA vitakuwa na mashine za kusafisha mahindi hivyo hakutakuwa na mateso
Mbegu za Ruzuku zitaanza kutolewana amewataka wakulima kutowauzia madalali mahindi adala yake wapeleke mahindi kitengo Cha Taifa Cha hifadhi ya chakula (NFRA) na amewataka wasiuze yote ili wale wa Dar es salaam bustani zao wapande Mahindi.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa Rais anaenda kuzindua Barabara ya Mbinga -Mbambabay kufunguka kwa barabara hiyo kunaenda kuhamsha Ruanda-Ndumbi pia wamepata mkandarasi hivyo kazi itaendelea.
Lukuyufusi -Mkenda kuelekea Msumbiji itaanza kujengwa na kwenda kumaliza changamoto hizo.