Baada ya tetesi kubwa za Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk huko Ubelgiji kuhitajika Levante, kuzidi kushika kazi, Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo amesema mambo bado hayajaa sawa.

Kisongo amefunguka na kueleza mazungumzo baina ya Levante na mabosi wa Samatta bado hayajaiva kutokana na klabu hiyo kutuma ofa ndogo ya euro milioni 4 pekee.

Meneja huyo amesema uongozi wa Genk umesema kiwango cha ofa ya fedha hiyo ambayo wametuma Levante hakiendani na thamani ya mchezaji hivyo wameombwa kuongeza dau jingine.

Samatta amekuwa katika fomu nzuri tangu ajiunge na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Congo.

Uwezekano wa Samatta kutimkia La Liga upo endapo pande zote mbili zitafikia mwafaka wa makubaliano ya fedha ili kumuuza straika huyo ambaye ni mmoja wa wanaotegemewa pake Genk.