Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari za treni ya reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro ambapo kuanzia Julai 5, abiria wataanza kutumia treni ya haraka (express train) isiyosimama vituo vya kati.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano, Jamila Mbarouk leo Julai Mosi imesema TRC itaendelea kuongeza safari za kwenda na kutoka Dar es Salaam na Morogoro.

“Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asibuhi na 01:10 jioni na itaondoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 01:30 usiku na treni ya kawaida itaondoka Dar es Salaam 03:30 asubuhi na saa 10:00 jioni na kwa Morogoro itaondoka saa 03:50 asubuhi na 10:20 jioni.

Nauli za SGR Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR (kawaida) zimewekwa kwa kuzingatia umbali wa safari na umri wa abiria. Kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12, nauli ni Tsh. 69.51 kwa kila kilomita. Watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12 watalipa nusu ya bei hiyo, yaani Tsh. 34.76 kwa kilomita. Watoto chini ya miaka minne watasafiri bure, lakini taarifa zao zitahitajika kurekodiwa.

Nauli kwa Abiria Wenye Umri Zaidi ya Miaka 12

Daraja la Kawaida:

SAFARIUMBALI (KM)NAULI (SHILINGI)
Dar es Salaam – Pugu191,000
Dar es Salaam – Soga514,000
Dar es Salaam – Ruvu735,000
Dar es Salaam – Ngerengere134.59,000
Dar es Salaam – Morogoro19213,000
Dar es Salaam – Mkata22916,000
Dar es Salaam – Kilosa26518,000
Dar es Salaam – Kidete31222,000
Dar es Salaam – Gulwe354.725,000
Dar es Salaam – Igandu387.527,000
Dar es Salaam – Dodoma44431,000
Dar es Salaam – Bahi501.635,000
Dar es Salaam – Makutupora53137,000

Nauli kwa Watoto Wenye Umri Kati ya Miaka 4 hadi 12

Daraja la Kawaida:

SAFARIUMBALI (KM)NAULI (SHILINGI)
Dar es Salaam – Pugu19500
Dar es Salaam – Soga512,000
Dar es Salaam – Ruvu732,500
Dar es Salaam – Ngerengere134.54,500
Dar es Salaam – Morogoro1926,500
Dar es Salaam – Mkata2298,000
Dar es Salaam – Kilosa2659,000
Dar es Salaam – Kidete31211,000
Dar es Salaam – Gulwe354.712,500
Dar es Salaam – Igandu387.513,500
Dar es Salaam – Dodoma44415,500
Dar es Salaam – Bahi501.617,500
Dar es Salaam – Makutupora53118,500

Masharti Kabla ya Safari Kuanza

LATRA imetoa masharti kadhaa ambayo yanapaswa kutimizwa kabla ya kuanza kwa safari za SGR. Masharti haya ni pamoja na:

  • Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa na leseni ya usafirishaji
  • Miundombinu ya reli na mabehewa kuwa na ithibati ya usalama
  • Matumizi ya mfumo wa utoaji tiketi za kielektroniki
  • Kuunganishwa kwa mfumo wa tiketi na mifumo ya LATRA
  • Uwepo wa watumishi waliothibitishwa na waliosajiliwa na LATRA