Serikali ya Rwanda imetangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji, ikidai kuwa Ubelgiji imekuwa ikiidhoofisha Rwanda wakati wa mzozo unaoendelea mashariki mwa DR Congo.

Ubelgiji nayo imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wa Rwanda, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Maxime Prevot, alieleza kusikitishwa na uamuzi huo, akisema unadhihirisha kutokuwepo kwa nia ya kushirikiana katika mazungumzo.

Hii inakuja baada ya Rais Paul Kagame wa Rwanda kuituhumu Ubelgiji kwa kuchonganisha Rwanda na mataifa mengine ili kuwekewa vikwazo kutokana na mzozo wa Mashariki mwa DR Congo.

Hivi karibuni, mataifa ya Ulaya yalewawekea vikwazo makamanda wa kijeshi wa Rwanda na DR Congo.