Serikali ya Rwanda imepeleka shehena ya misaada ya kibinadamu zaidi ya tani 19 za chakula,vyakula vya watoto, dawa na vifaa vya matibabu kusaidia wananchi wa Gaza.
“Rwanda itaunga mkono jitihada za kimataifa katika kutoa misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa ukanda wa Gaza wanaoendelea kuteseka na mapigano ya vita”, taarifa ilisema,
Taarifa ilieleza kuwa “Rwanda itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha kuimarisha ulinzi wa maisha ya raia wa Gaza,” taarifa ilisisitiza.
Maeneo mengi ya Palestina yameendelea kukaliwa kwa mabavu na Israel ambapo Ofisi ya umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA) ilitoa wito wa kuchangia dola bilioni 2.822 kwa mashirika ya umoja wa mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa (INGO) na washirika wa NGO kushughulikia zaidi mahitaji ya dharura ya zaidi ya watu milioni tatu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ya kati , katika kipindi cha miezi tisa, kuanzia Aprili hadi Desemba.