Zaidi ya makanisa 4,000 yamefungwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita nchini Rwanda kwa kushindwa kuzingatia kanuni za afya na usalama, ikiwa ni pamoja na kutozuiliwa ipasavyo.

Hatua ihiyo imeathiri zaidi makanisa madogo ya Kipentekoste – baadhi yanafanya ibada nje ya mapango au kwenye kingo za mito.

“Hii haifanywi kuwazuia watu kusali bali kuhakikisha usalama na utulivu wa waumini,” Waziri wa Serikali ya Mitaa Jean Claude Musabyimana aliviambia vyombo vya habari vya serikali.

Ni msako wa kwanza mkubwa tangu sheria ilipobuniwa miaka mitano iliyopita kudhibiti maeneo ya ibada.

Please follow and like us:
Pin Share