Rais wa Kenya William Ruto amewateua vigogo wanne wa upinzani katika baraza lake la mawaziri, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja wa maandamano ya kupinga serikali.

Rais wa Kenya William Ruto amewateua vigogo wanne wa upinzani katika baraza lake la mawaziri, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja wa maandamano ya kupinga serikali.

Ruto alitangaza majina ya mawaziri 10 kuwa sehemu ya mageuzi ya baraza lake, ikiwemo wanasiasa wanne ambao ni washirika wa karibu wa kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga.

Rais Ruto amemteua gavana wa zamani wa kaunti ya Mombasa, Hassan Ali Joho kuwa waziri wa madini na masuala ya  bahari. John Mbadi wa chama cha ODM ndiye atakayekuwa waziri mpya wa fedha.

Aliyekuwa waziri wa usafiri na miundombinu Kipchumba Murkommen, amehamishwa katika wizara inayoshughulikia masuala ya vijana, uchumi wa ubunifu na michezo. Ruto ameahidi kuyataja majina mengine ya mawaziri muda mfupi ujao.

Please follow and like us:
Pin Share