Hatima ya Kamati
Kutokana na kuwapo tuhuma za rushwa za waziwazi katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, kuna uwezekano wa kufanyika mambo matatu. Mosi, ni kumsimamisha Badwel na wenzake wanaotuhumiwa kuomba rushwa. Kamati ya Haki, Maadili na Kinga ina mamlaka ya kumwadhibu mbunge aliyekiuka maadili.

Pili, Badwel kuvuliwa ubunge. Hilo linawezekana zaidi kama chama chake CCM katika kujisafisha na kujijengea taswira nzuri katika jamii, kitaamua kuchukua uamuzi huo mgumu. Tatu, ni kuvunjwa na kusukwa upya kwa Kamati hiyo.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Spika ana mamlaka ya kuvunja na kusuka upya Kamati. Hilo linawezekana hasa wakati huu ambao kuna wabunge kadhaa wapya.