Ndege ya Shirika la Ndege la ‘Turkish Airlines’ lenye makao makuu yake nchini Uturuki imeripotiwa kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy jijini New York nchini Marekani mara baada ya nahodha wa ndege hiyo, Ilcehin Pehlivan kufariki dunia akiwa ndani ya ndege hiyo, maofisa wa shirika hilo wanaeleza.

Ndege hiyo aina ya Airbus A350-900 iliyokuwa ikitoka mji wa Seattle ndani ya Washington DC kuelekea Mji Mkuu wa Uturuki, Istanbul lakini kwa maamuzi ya haraka ilichukua mwelekeo wa haraka kuelekea New York, hii ni kulingana na taarifa kutoka tovuti ya ufuatiliaji wa ndege Flight Aware.

Ilcehin Pehlivan ,59, alizidiwa wakati wa safari, msemaji wa shirika hilo, Yahya Ustun, aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter.

TK204 sefer sayılı Seatle- İstanbul seferini icra eden TC-LGR kuyruk tescilli Airbus 350 tipi uçağımızın Kaptan Pilot’u İlçehin PEHLİVAN, sefer esnasında baygınlık geçirmiştir. Kaptanımıza uçakta yapılan ilk doktor müdahalesi sonuçsuz kalınca 1 kaptan ve 1 yardımcı pilottan…

“Baada ya jaribio lisilofanikiwa la kutoa huduma ya kwanza, wafanyakazi wa ndege, wakiwemo rubani mwingine na rubani msaidizi, waliamua kufanya maamuzi ya dharura, isivyo bahati rubani alifariki dunia kabla ya kutua,” msemaji amefafanua.

Please follow and like us:
Pin Share