Manchester United imethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo ameondoka katika klabu hiyo kwa mara ya pili baada ya mkataba wake kuvunjwa na kutekelezwa mara moja kwa ‘makubaliano ya pande zote’.
Hiyo inakuja siku chache baada ya mahojiano yaliyoonekana kuwa ya kichochezi ambayo Ronaldo alitoa kwa Piers Morgan na TalkTV, ambapo aliikosoa vikali klabu hiyo.
Kupitia taarifa ya Klabu iliyotolewa Jumanne Novemba 22, 2022 imeeleza kuwa “Cristiano Ronaldo ataondoka Manchester United kwa makubaliano ya pande zote mbili, na kutekelezwa mara moja,”
“Klabu inamshukuru kwa mchango wake mkubwa katika vipindi viwili vya Old Trafford, akifunga mabao 145 katika mechi 346, na inamtakia heri yeye na familia yake kwa siku zijazo.
Kila mtu katika Manchester United anabakia kulenga kuendeleza maendeleo ya timu chini ya Erik ten Hag na kufanya kazi pamoja kuleta mafanikio uwanjani.”
Ni Siku chache zimepita tangu Ronaldo aliposema alihisi kusalitiwa na Manchester United na kwamba uongozi wa klabu hiyo ulikuwa haumtaki tena na kujaribu kumuondoa kwa nguvu.