SMZ imeibiwa mabilioni
576. Benki Kuu yaTanzania ibuni mbinu za kupunguza matumizi ya fedha taslim katika uchumi wetu. Sheria zote muhimu zifanyiwe marekebisho ili kuwabana wale wote wanaolimbikiza fedha majumbani mwao.
577. Kampuni au biashara inaposajiliwa, wanaohusika na kusajili watoe taarifa kwa Mamlaka ya Mapato mara moja. Mwenye biashara au kampuni kama hajachukua leseni kwa kipindi cha mwaka mmoja aingizwe kwenye orodha ya walipa kodi.
578. (i) Mamlaka ya Mapato iwe na ofisi za malalamiko dhidi ya utozaji kodi holela, ukwepaji kodi kwa washindani na kwa maafisa ambao watawatendea wateja vibaya.
(ii)Mamlaka ya Mapato iwe na ofisi au kamati za kusikiliza rufani za walipakodi. Rufani hizo zisikilizwe ndani ya siku 14 baada ya kuwasilisha rufani na pasiwepo na haja ya kulipa sehemu yoyote ya kodi kabla ya rufani kusikilizwa atakayeomba rufani atakiwe kulipa ada ya kukata rufani.
579. Tume ya Mtei pamoja na Tume ya Mramba zimependekeza utozaji kodi kwa majengo yanayopangishwa katika miji. Misingi ya utozaji kodi hii uwe ni thamani ya jengo. Tume inaafiki kwamba ni vizuri mapendekezo hayo yakatekelezwa sasa ili kuboresha makusanyo ya mapato ya Serikali.
600. (i) Serikali iandae utaratibu utakaotumika kuwatoza wakulima na wafugaji kodi ya mapato ili kupanua wigo wa kodi ya mapato.
(ii)Serikali ibuni mfumo wa kuwapatia maskani maalum ya biashara wale wote wanaofanya biashara barabarani na barazani bila ya leseni.
(i) Halmashauri za jiji, miji na wilaya zibuni mbinu za kuwatoza watembezaji bidhaa ada ya leseni za biashara ili kujenga utamaduni wa kufanya biashara kulingana na sheria.
(ii) Serikali za mitaa zihamasishe Serikali za vijiji kukusanya Kodi ya Maendeleo kwa kuziachia asilimia ya mapato yatakyaokusanywa na vijiji hivyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
KIAMBATISHO A
MAKUSANYO YA KODI KWA KIPINDI CHA 1990/91 – 1994/95
|
1990/91 |
1991/92 |
1992/93 |
1993/94 |
1994/95 |
Total Revenue |
137,092.9 |
173,565.5 |
164,109.9 |
237,897.0 |
311,280.0 |
Tax Revenue |
118,257.8 |
153,355.6 |
146.419.0 |
221,258.0 |
270,940.0 |
Customs & Excise |
56,319.9 |
51,638.6 |
36,706.0 |
57,819.0 |
81,318.0 |
Income Tax |
32,413.0 |
40,143.0 |
45,455.0 |
63,026.0 |
86,684.0 |
Sales Tax |
20,171.6 |
44,862.2 |
41,047.0 |
57,578.0 |
72,645.0 |
Others Taxes |
9,353.3 |
16,711.8 |
23,211.0 |
42,835.0 |
39,293.0 |
KIAMBATISHO B
WAKALA WA FORODHA WALIOFUNGIWA LESENI KUTOKANA NA MATUMIZI YA HATI BANDIA KUTOA MAKASHA (CONTAINERS) MANANE AMBAYO YALIKAMATWA |
||
KAMPUNI |
WAKURUGENZI |
SABABU |
1. TARU (R ) RUSUA Co. Box 46626 DSM |
Yisambi Robert Mboma Shali Robert Mboma Yisega Yisambi Nicodemus |
Kukwepa Ushuru wa Forodha kwa kutumia hati bandia kuondoa mali bandarini Ushuru – Shs.18,522,845/- Sales Tax Shs. 12,920,729/- |
2. Marik Freight Box 4614 DSM |
Josephat J. Mwakitwange Ramesh Jayantilal Patwa |
Kukwepa Ushuru wa Forodha kwa kutumia hati bandia Ushuru: Shs. 26,597,935/- Sales Tax: Shs. 13,805,747/- |
3. Truck Freight Box 16552 DSM |
Jamal A. Ahmed Abdallah A. Ahmed |
Kukwepa kodi kwa kutumia hati bandia Ushuru: Shs. 7,627,190/- |
KIAMBATISHO C
SUMMARY OF QUANTITIES OF PETROLEUM PRODUCTS DUMPING FOR THE PERIOD OF JUNE 1994 TO 1995
Company |
MSP (lts.) |
JET A-1 (lts.) |
IK (lts.) |
GO (lts.) |
FO (lts.) |
SUM (lts.) |
AGIP
DP-DSM
BP-MBEYA
BULKOIL
GAPCO
CALTEX
MOBIL
TOTAL (T) |
2,779,203
14,922,743
6,996,524
1,716,014
–
1,876,091
10,639,093
7,376,466
|
141,208
5,573,255 –
44,645
2,040,983
–
757,000
57,443 |
741,542
94,174 –
46,454
–
185,763
274,433
1,648,111 |
7,070,397
16,451,766
5,923,661
1,605,730
327,733
4,690,524
11,874,085
12,374,085 |
72,832
–
100,330
–
–
–
50,245 |
10,805,182
37,041,908
12,920,135
3,513,673
2,368,766
6,752,378
23,444,611
22,006,413 |
SUM |
46,306,134 |
8,614,504 |
2,990,477 |
60,718,099 |
233,907 |
118,353,121 |
AMOUNT INVOLVED AS PER PRICE STRUCTURE
|
MSP (Tshs.) |
JET A-1 (Tshs.) |
IK (Tshs.) |
GO (Tshs.) |
FO (Tshs.) |
SUM (Tshs.) |
T.E.F. P.S.R.F. |
80,072,567 |
3,510,704 |
5,171,133 |
104,993,737 |
611,067 |
214,359,228 |
Sales Tax |
23,153,067 |
8,614,504 |
1,495,239 |
30,359,050 |
223,907 |
63,845,766 |
Ex. Duty |
1,774,932,639 |
53,937,132 |
18,798,737 |
0 |
1,478,615 |
1,849,147,123 |
F.O.B. Diff. |
470,403,178 |
9,184,374
75,253,290 |
26,060,061 |
435,785,940
435,785,940 |
2,521,517
1,955,973 |
1,003,955,670
965,290,973 |
Road Toll |
427,667,246
1,736,480,025 |
0 |
24,683,522
0 |
283,928,713 |
|
4,013,408,738 |
|
4,512,708,722 |
230,500,006 |
76,154,294 |
3,283,853,379 |
6,791,099 |
8,110,007,497 |
T.E.F = Transport Equalization Fund; P.S.R.F= Petrol Sector Rehabilitation Fund
KIAMBATISHO D
MIFANO YA WAKALA WA MIZIGO WALIOFUNGIWA LESENI KWA KUSHINDWA KUTOA TAARIFA KUHUSU USAFIRISHAJI WA TRANSIT GOODS
KAMPUNI |
WAKURUGENZI |
SABABU |
1. Jambo Freight P.O. Box 4614 DSM |
G. Mahinda, J. Mzuanda |
Kushindwa kuwasilisha taarifa za kuonyesha kama mali waliyokuwa wapeleke Transit imepelekwa inakohitajika Ushuru – Revenue Liability BIF Shs. 12,620,374/- |
2.Oriental C & F P.O. Box 71305 DSM |
Mrs. Hamida Thabit Ali Senyange |
Kushindwa kutoa taarifa kama mali iliyokuwa isafirishwe kwenda nchi jirani imefika inakohitajika – Ushuru Shs. 622,872,542/- |
1. Trans Ocean (Uganda Ltd), P.O Box 9770 DSM |
Mr. Kagwa E. Okuraja |
Kushindwa kuwasilisha taarifa kama mali waliyokuwa wapeleke nchi jirani imefika inakohitajiwa. Ushuru – Revenue Liability Shs. 268,301,536/- |
2. Chanya Investment P.O. Box 60672 DSM |
Donald Chacha F. Oluoch Nyarara |
-do- Revenue Liability Shs. 56,036,256 |
3. Overseas Trade Ways P.O. Box 70489 DSM |
Andrew Kagwa Bigirimfura A. E. hakizimfura |
-do- Revenue Liability Shs. 10,701,268/- |
4. Inter Africa C & F Dar es Salaam |
Godfrey Sindani Charles Nkuba Aron Nkuba |
-do- Revenue Liability Shs. 12,620,374/- |
5. Agree Group Agencies |
Hashim Rungwe |
Revenue Liability Shs. 392,000,000/- |
KIAMBATISHO E
Hill Top Hotel and Tours Ltd inayomilikiwa na Mohsin Abdallah na Hitesh P. Arjun ilipewa Certificate of Approval Enterprise na Kituo cha Uwekezaji Rasilimali tarehe 3/1/1991. Baadaye watu hoa walianzisha kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel iliyosajiliwa tarehe 2/4/1992 na ambayo ilirithi ‘Certificate of Approval Enterprise iliyokuwa imetolewa kwa kampuni ya Hill Top Hotel and Tours kuendeleza ujenzi wa Hotel ya Kitalii ya Kigoma. Kampuni hii mpya inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Hitesh Arjun na Deusidedit Kisisiwe. Wamiliki hawa pia wanamiliki makampuni mengine ama kwa pamoja au mmoja wa kama ifuatavyo.
(i) SHENIS COMMERCIAL LTD, inayoshughulika na mauzo ya nguo, vitambaa na vipuri vya magari na mashine inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Mrs. Nargis Mohsin Abdallah na Deusdedit Kisisiwe. Kampuni hii ilisajiliwa tarehe 27/7/1988.
(ii) TILE AND TUB LTD iliyosajiliwa tarehe 7/12/1992 inashughulikia na biashara ya vifaa vya ujenzi, umeme, pombe na madawa na inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Deusidedit Kisisiwe na Tariq Mirza.
(iii) FIVE WAYS CLEARING AND FORWARDING AGENCY iliyosajiliwa tarehe 23/10/1992 kwa ajili ya kuondoa mizigo bandarini na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia mbalimbali biashara ya vipuri na vifaa vya ujenzi uchimbaji na uuzaji wa madini nchi za nje inamilikiwa na Triphon Maji na Deusdedit Kisisiwe.
(iv) ROYAL FRONTIER (T) LTD iliyosajiliwa tarehe 7/3/1994 kwa ajili ya uwindaji wa kitalii na usafirishaji wa watalii inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Deusidedit Kisisiwe na Rashid Omar.
(v) GAME FRONTER (T) LTD na MNM Hunting Safaris Ltd inafanya shughuli zinazofanana na zile za Royal Frontier na inamilikiwa na Mr. Mohsin Abdallah, Mr. Abdikadir Mohamed na Mr. Ahmad Muhidin.
Shenis Commercial Ltd ndiyo kampuni ya kwanza kisha ikafuatiliwa na Kigoma Hill Top. Baadaye makampuni mengine yaliibuka haraka haraka jambo linaloashiria kwamba yalitokana na Kigoma Hill Top na yanafanya shughuli zake kwa kushirikiana.
Vifaa vilivyoagizwa na Kigoma Hill Top na kusamehewa kodi ni vingi kuliko mahitaji ya hoteli kwa mfano kampuni iliagiza vigae vya sakafu 27,248, containers 3 za marumaru zenye ujzao wa mita za mraba 3264.8, magodoro 120 na taulo 4000 wakati hoteli ina vitanda 60 tu.
Aidha iliruhusiwa kuagiza boti tatu na injini nne (outboard engines) na kufanya Hotel huyo kuwa na boti 7. Idadi hii ya boti ambazo imeelezwa kwamba zitatumika kwa uvuvi wa kitalii ni nyingi sana ikilinganishwa na idadi ya vyumba vya Hotel hiyo inawezekana zitatumiwa kwa shughuli nyingine. Vifaa vya ziada inaaminiwa viliuzwa na makampuni mengine yanayomilikiwa na wakurugenzi wa Kigoma Hill Top Hotel.
Taarifa ya IPC inaonyesha kwamba ingawa kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel ilipatiwa misamaha ya kodi. IPC haikuona na kupendekeza aina ya vifaa vya ujenzi wa Kigoma Hill Top Hotel vinavyotakiwa kusamehewa kodi. Wakurugenzi wa kampuni walikuwa wanawasiliana na Hazina moja kwa moja kuanzia mwaka 1991 hadi Julai 1995 walipoanza kupitisha maombi ya misamaha hiyo IPC.
Hata hivyo baadhi ya vifaa ambavyo vilisamehewa kodi na Hazina havikusastahili kusamehewa kodi. Kwa mfano kampuni ilisamehewa kodi Magari Na. TZF 5059 Toyota S/Wagon, TZF 8455 Toyota L/Cruiser, TZF 8612 Landcruiser S/Wagon na TZF 6001 ambalo ni gari ya kifahari ya aina ya Mercdes Benz Sportscar, na ndege moja.
Ijapokuwa magari na ndege hiyo vyote vilisamehewa kodi chini ya mradi wa Kigoma Hill Top yamekuwa yanatumika na kampuni zao nyingine hapa Dar es Salaam na Kigoma. Kwa mfano gari Na. TZF 8454 lililoandikishwa tarehe 16/6/1994 kama mali ya Kigoma Hill Top, chini ya Import Declaration mwagizaji alikuwa Royal Frontier na Import Entries zilionyesha Kigoma Hill Top.
Kampuni hii ilikuwa iagize ndege mwaka 1995 na ikasemehewa kodi kwa barua Kumb. Na TYC/1/150/9/176/7. Uchunguzi umeonyesha kwamba hakuna ndege iliyosajiliwa hapa nchini kwa jina la kampuni hiyo lakini kampuni ya Game Frontiers ina ndege yenye namba za Usajili 5H-GFT (Cesna 206) iliyosajiliwa mwaka 1995.
Uchunguzi pia unaonyesha kwamba kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel inatumia sana ndege hiyo kwa kuwapeleka watalii na wageni huko Kigoma Hill Top Hotel ingawa haina leseni ya biashara ya usafiri wa anga. Ifuatayo ni taarifa ya Idara ya Forodha kuhusu misamaha ya Kodi iliyotolewa na Hazina kwa ajili ya Magari, marumaru, sanitary ware na vifaa vya umeme.
Kifaa |
Kibali cha Hazina |
CIF Value |
Import Duty |
Sales Tax |
Jumla ya misamaha |
Tan 389 Jan 94 1 Toyota L/cruiser |
TYC/1/150/9/176/9 of 20/9/93 |
24,493,406.81 |
9,796,960.73 |
13,372,852.94 |
23,269,813.67 |
Tan 515 Jan 1994 1 Toyota L/Cruiser |
-do- |
26,515,578.58 |
5,303,334.12 |
7,995,001.17 |
13,258,335.29 |
Tan 398 of March 94 I M/Benz |
-do- |
42,075,345.09 |
16,840,138.04 |
22,973,138.42 |
39,813,276.46 |
Tan 202 of Feb 1994 Sanitary ware |
TYC/1/150/9/176/7 of 9/7/93 |
9,927,493.38 |
2,678,250.58 |
3,481,723.25 |
6,159,973.38 |
Tan 18 of Dec. 1993 Ceramic tiles |
-do- |
11,702,352.83 |
3,510,707.22 |
4,563,918.02 |
8,074,625.24 |
Tan 1305 of Aug. 1993 Lighting Fixtures |
-do- |
7,194,846.44 |
2,158,451.85 |
2,805,995.68 |
4,964,447.53 |
JUMLA |
|
|
40,287,842.54 |
55,152,629.48 |
95,440,472.02 |
Tume imezungumza na mmoja wa wamilikaji wa kampuni ya Kigoma Hill Top Bw. Deudedit Kisisiwe lakini maelezo aliyoyatoa kuhusu tuhuma hizo hayakuridhisha. Tume inaamini kwamba;
(i) Bwana Mohsin Abdallah na wenzake, hasa Deusdedit Kisisiwe wamefungua kampuni nyingi za biashara na kuomba misamaha ya kodi kwa kampuni moja ya Kigoma Hill Top Hotel Kampuni imeagiza vitu vingine vilivyosamehewa kodi na kuvitumia au kuviuza kupitia makampuni yao mengine ambayo hayakupata misamaha ya kodi.
(ii) Wafanyabiashara wamekuwa wanawatumia viongozi wa Serikali katika kuficha maovu yao. Kwa mfano Kampuni ya Fiveways Clearing and Forwarding Agency ilimpa hisa Bw. Tryphon Maji aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es salaam na hivyo alikuwa habughudhiwi na Polisi anapofanya vitendo kinyume na kanuni na taratibu.
Katika kampuni ya Royal Frontier (T) Ltd hisa zimetolewa kwa Ahmed Muhidin ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori Bw. Muhidin Ndolanga. Hisa hizi zimetolewa kwa wakubwa hawa kama vivuli (cover) ili waweze kuyapatia makampuni haya vitalu vya Uwindaji pamoja na kurahisisha shughuli za Uwindaji.
(iii) Bw. Mohsin Abdallah na Kisisiwe wanapenda kuwatumia viongozi kama chambo katika biashara zao ili waweze kuvuka kikwazo chochote kile kitakachokwamisha biashara zao.
KIAMBATISHO F
MUHTASARI WA KODI YA ZIADA ILIYOKADIRIWA NA KUKUSANYWA NA IDARA YA FORODHA BAADA YA TANS KUTOLEWA NA SGS NA INCHCAPE |
|
KIPINDI |
MAKUSANYO |
Mwaka wa Fedha 1994/95 |
Shs. 908,306,784.00 |
Mei 1995 |
Shs. 218,098,558.00 |
Juni 1995 |
Shs. 128,092,558.00 |
Julai 1995 |
Shs. 70,761,300.00 |
Agosti 1995 |
Shs. 165,367,620.00 |
September 1995 |
Shs. 86,897,504.00 |
Oktoba 1995 |
Shs.125,494,275.00 |
Novemba 1995 |
Shs. 128,977,294.00 |
Desemba 1995 |
Shs. 70,397,848.00 |
Januari 1996 |
Shs. 729,252,949.00 |
JUMLA |
Shs. 2,285,459,533.00
|
KIAMBATISHO G
REVENUE RECONCILIATION SUMMARY SERVICES OF INCHCAPE OCTOBER 1995 TO FEBRUARY 1996
Month |
Duties and taxes assessed |
Value of exemptions |
Duties and taxes payable |
Total collections |
% of 5 to 4 |
1 |
2 |
3 |
4 |
5 |
6 |
Oct. 1995 |
5,218,726.1 |
2,560,640.7
1,808,312.0 |
2,658,085.4
2,515,790.0 |
1,119,381.8
1,112,887.0 |
42
44 |
Nov. 1995 |
4,324,102.0
|
1,359,593.0 |
1,479,202.0 |
1,084,608.0 |
73 |
Dec. 1995 |
2,838,795.0
|
2,355,761.5 |
2,668,637.2 |
1,175,929.8 |
44 |
Jan. 1996 |
4,024,398.7
|
7,084,307.2 |
9,321,714.6 |
4,492,806.6 |
48 |
TOTAL
|
16,406,021.8 |
|
|
|
|
Chanzo: Inchcape Testing Services – Pre-shipment Inspection Monthly Reports – October 1995 – February 1996.
KIAMBATISHO H
WIZI WA USD 434,716.23 KATIKA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR
Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar Bw. Naushad Mohamed Suleiman alikuwa na A/C ya fedha za kigeni katika Benki ya Wananchi wa Zanzibar. Katika kipindi cha tarehe 13 Julai 1991 mpaka Februari,1992 aliweza katika nyakati mbali mbali kutoa jumla ya USD 434,716.23 bila fedha hizo kuingizwa kwenye akaunti yake na hivyo kupelekea akaunti yake kuwa ‘overdrawn.’
Benki ilichukua hatua za kumshawishi mteja kusawazisha madeniyake na alikataa. Bodi ya PBZ iliamua kumshtaki na ikawasilisha shauri hilo Polisi kwa upelelezi wa kina na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Upelelezi wa kesi hii ulifanyika kwa pole pole sana baadaye Polisi wakaeleza kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kumshataki mfanyabiashara huyu.
Hata hivyo, PBZ ilieleza kwamba yenyewe ina ushahidi tosha wa kuweza kufungua kesi ya madai dhidi ya mteja huyu. PBZ ilifungua kesi ya Madai Na. 13 ya mwaka 1995. Baada ya kufunguliwa kwa kesi hiyo Serikali ya Mapinduzi ilitoa shinikizo na kwa barua ya Wizara ya Fedha ya Februari 15, 1996 Benki iliagizwa kufuta kesi hiyo na kutafuta njia nyingine kufidia hasara iliyopatikana.
Tume ilifanya uchunguzi wa suala hili ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya PBZ na maoni ya Tume ni kwamba haikuwa sahihi kwa Serikali kuingilia suala hili lisifikishwe mahakamani.
Je, unafahamu Jaji Warioba katika ripoti hii aliyoiandaa mwaka 1996 alipendekeza ni kuhusu eneo la ardhi? Ingawa ripoti hii imeandikwa mwaka 1996, inaendelea kuwa na maudhui yenye uhalisia na yenye kuonyesha upungufu ule ule hadi sasa na hivyo inastahili kufanyiwa kazi. Usikose JAMHURI wiki ijayo. Mhariri.