Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia,Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewaasa Wanachalinze kuondoa tofauti ili kufikia maendeleo ya kweli wanayoyahitaji.

Ridhiwani ambae pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora alitoa rai hiyo wakati, akizungumza na wananchi wa Kata ya Bwilingu na Ubena kwa nyakati tofauti kwenye ziara yake.

Aliwasisitiza kuyakimbilia maendeleo badala ya kuweka tofauti za kiitikadi,ama makundi .

Katika ziara hiyo Kikwete amezindua program ya ukusanyaji taka yenye lengo la kutengeneza mazingira na kufanya Mji wa Chalinze kuwa safi .

Pamoja na hilo, amekagua miradi ya maendeleo,ujenzi wa Mabweni, Zahanati kabla ya kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Ubena zomozi na baadae Lulenge katika kijiji cha Kaloleni mjini hapo.

Ridhiwani anaendelea na ziara yake ya jimbo akikagua miradi mbalimbali na kuzungumza na wananchi kwenye kata za Chalinze.