Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Kilosa

Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Ridhiwani Kikwete amewahimiza viongozi wa Wilaya ya Kilosa kusimamia mpango wa matumizi ya mashamba 11 aliyoyakabidhi mwishoni mwa wiki , wilayani humo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Naibu Waziri Kikwete amewashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kushirikiana na Rais Samia katika maendeleo.

“Na hii ndiyo sababu Rais ameona kipaumbele kikubwa ya mashamba hayo kiwe ni wananchi ambao amewaomba mjiunge kwenye vikundi vya Ushirika ili mtumie kwa ajili ya Kilimo chenye tija” alifafanua Waziri Kikwete.

Kwa upande wa wakazi hao, wamemshukuru na kumpongeza Rais kwa kuwapatia mashamba hayo na wakaahidi kuyatumia kama walivyoelekezwa.

Hata hivyo Ridhiwani ameeleza ziara yake inayohusiana na utatuzi wa migogoro ya ardhi itaendelea baada ya Zoezi la Sensa tarehe 23 Agosti 2022.