đź“ŚMatumizi bora ya nishati ya kupikia kupewa kipaumbele
đź“ŚElimu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme yatolewa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unashiriki katika Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati 2024 unaofanyika jijini Arusha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.
REA imeungana na wadau mbalimbali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo (SADC) kushiriki katika mkutano huo muhimu.
Aidha, wadau mbalimbali wameendelea kuvutiwa na huduma zinazotolewa katika banda la REA ikiwemo elimu sahihi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.
Kupitia mkutano huo, REA imetoa elimu kwa wadau mbalimbali wa nishati ya umeme ili kuwahakikishia Watanzania upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini