Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma
WakalaAm wa Nishati Vijijini (REA), umeanza
kutekeleza Mradi wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia kwa utaratibu wa utoaji ruzuku ambapo umewezesha usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia (LPG) 71,000 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.
Hayo yamesemwa leo Agosti 18, 2023 jijini hapa na Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Mhandisi Hassan Saidy alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya REA.
Amesema usamazaji wa mitungu ya Gesi utaenda Sambamba na majiko banifu 200,000 (laki mbili) katika maeneo ya vijijini.
“Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Jumla ya fedha takribani TZS bilioni 10 zimetengwa kwaajili ya kufanikisha mradi huo,” amesema mkurungezi huyo.
Amesema wanatekeleza Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia ya kupikia (CNG) katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani (Pembezoni mwa Mkuza wa Bomba Kuu la Kusafirisha Gesi Asilia).
Utekelezaji wa mradi huu utahusisha REA na TPDC; Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Jumla ya TZS bilion 20 zinatarajiwa kutumika;
“Mradi huu utahusisha ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi asilia (CNG) lenye urefu wa km 44.4 (Mnazi Mmoja – Lindi (km 22.9) na Mkuranga – Pwani (km 21.5));Jumla ya nyumba/wateja 980 kunufaisha (Mnazi Mmoja – Lindi, wateja 451 na Mkuranga-Pwani, wateja 529),” Amesema.
Mradi wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Utaratibu wa Malipo kwa Matokeo (RBF)Serikali kupitia REA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) imetenga Dola za Kimarekani (USD Milioni 6) kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa majiko banifu ya kupikia;
Aidha Amesema Takribani Majiko 200,000 yanatarajiwa kusambazwa katika maeneo mbali mbali ya vijijini na vijiji miji (Peri Urban) Tanzania bara.
WANUFAIKA:
Ameeleza wanufaikaji watakuwa ni Wazalishaiji na Wasambazaji Wadogo wa Ndani wa majiko banifu.
“Lengo letu ni Kukuza na kuboresha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ambapo kwa sasa, Wakala upo kwenye mchakato wa uandaaji wa taratibu na kanuni za utoaji wa ruzuku ,” amesema