Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Manyara
Unapozungumzia mgogoro wowote wa ardhi hapa unatakiwa kwanza kabisa kujua nini maana halisi ya ardhi ambayo ni sehemu ambayo ipo juu na chini ya uso wa nchi pamoja na mimea inayoota au kupandwa juu yake, kama majengo, mawe, milima, ambapo ardhi hii inaweza kumilikiwa na mtu binafsi, kundi la watu, Taasisi na kusimamiwa na mamlaka mbalimbali.
Pia unapozungumzia mgogoro wa ardhi unatakiwa kwanza kabisa ni hali ya kutofautiana baina ya pande mbili au zaidi juu ya umiliki, matumizi, upatikanaji, usimamizi wa ardhi pamoja rasilimali zilizopo katika ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga akiendelea na ziara yake ya siku nne wilayani Simanjiro mkoani humo yenye lengo la kuona na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo huku akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hapa anaingia katika Kijiji cha Loiborsoit A ambapo anakutana na mgogoro wa ardhi Na. 24 uliodumu takribani miaka 9 iliyopita baina ya wananchi na Mwekezaji wa ardhi na.24 ambapo Mwenyekiti wa Kijiji hiko Langai Sarash anapata wasaa wa kumuelezea Mkuu wa Mkoa juu ya mgogoro huo.
Sarash anasema” Tunayo ekari kubwa katika shamba la na.24 zenye jumla ya ekari zipatazo 1,784 ambayo bado inamilikiwa na Mwekezaji badala ya kurudishwa Kwa wananchi tangu Mwaka 2016, lakini mpaka sasa hivi bado shamba hilo linafjidi kuleta mgogoro mkubwa na kupoteza amani Kwa wananchi wa Kijiji cha Loiborsoit A” anasema Sarash.
Anasema ndani ya shamba hilo wanafuga wanyamapori kinyume nataratibu na inajulikana, hivyo ” Mh Mkuu wa Mkoa kupitia hii ziara Yako ya kuwa hapa na sisi leo, tunakuomba uingilie kati mgogoro huu ili hizi hekari 1,784 ziweze kurudi na kukabidhiwa kwa wananchi na kunitumia, na hatimaye mgogoro huo Sasa uweze kuisha kabisa, na wananchi waweze kuendelea vema na shughuli zao za Maendeleo ” anasema Sarash.

Aidha kufuatia mgogoro huo hapa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Sendiga sasa anaeleza ” Labda kama baadhi ya viongozi wenu hawajawaambia ninyi ukweli wanawadanganya sasa Mimi nataka nikwambie ukweli na twende kwenye suluhish, na hii kitu nimeifanya kwenye mkoa mzima na naendelea kufanya, kwa sababu najua kuna baadhi ya maswali yameulizwa pasipo watu kuwa na uelewa mkubwa wa kutosha kuwa baadhi ya maeneo yaliuzwa wananchi wakiwa hawakusaidiwa kuambiwa nini kitatokea baadaye” ndivyo anavyoanza kuzungumza Queen Cuthbert Sendiga.
Sendiga anafafanua kuwa shamba na. 24 liliuzwa kwa mwekezaji na alilinunua kihalali, ni mali yake halali ndio maana ana miliki na uthibitisho anao ( Documents zote halali za umiliki anazo, lazima kwanza tukubali ukweli huo, viongozi tuwe tunawasmbia wananchi ukweli ingawa wakati mwingine ukweli Huwa unauma.
” Shamba na.24 ni mali ya Mwekezaji ni la kwake aliuziwa kihalali ana documents zote, alilipa pesa ni mali yake lakini miaka imeenda yawezekana ukubwa wa shamba alilopewa kuwa ni kubwa kuliko matumizi anayotumia inawezekana kabisa lakini ni la kwake haliondoi kwamba si la kwake ” anasema Sendiga.
Aidha anasema yeye kama Mkuu wa Mkoa hana Mamlaka ya kumnyan’ganya shamba lile mwekezaji wakati ana hati mmiliki, lakini Kwa kutumia busara, hekima, na uungwana tunaweza kukaa naye mwekezaji mezani tukapata kuzungumza naye na kupata kipande tukaendelea kufanya na maisha yetu yakaendelea lakini sio kumlazilisha, sasa ndugu zangu kitu ambacho tumekosea ni kulazimisha mali ya mtu iwe yetu huku mkifanya fujo, kuingiza mifugo kule ndani, kufanya heka heka na vita hilo ni kosa kubwa sana

HATUA YA KUCHUKUA / MAAMUZI YA RC SENDIGA KWA DC FAKII LULANDALA
” Mheshimiwa DC hili shamba ni kubwa sana, mwekezaji alisharidhia kutoa hizi heka 1,784 zirudi kwa wananchi , sasa kilichokua kinatakiwa hapa ni utaratibu wa kisheria ufanyike, nyie wananchi mliposikia tu kuna hizi heka 1,784 mkaanza kupeleka mifugo na kufanya vurugu kule kwenye shamba la mwekezaji, ndipo mwekezaji akasema sitoi tena kwa kuwa nazimiliki kihalali” anafafanua Sendiga.
Aidha anaongeza kwakua mwekezaji alisharidhia kutoa hizi heka 1,784 kwenda Kwa wananchi hapa sasa natoa maelekezo ” wewe Mheshimiwa Dc na wajumbe wachache wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu wa ardhi kaeni tena na mwekezaji kwa ajili ya hizi ekari 1,784.
” Mimi kama mkuu wenu wa mkoa moja ya kazi yangu kubwa ni kusimamia sheria, kanuni , taratibu, na miongozo inayoongoza nchi hii, sipo hapa kwaajili ya kutengua sheria, na sina mamlaka ya kuwa juu ya sheria, kama ambavyo hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria , kwahiyo siwezi kutamka kwamba nendeni mkachukue hili shamba kwa kuwa najua kuwa hili eneo ni la mtu analimiliki kihalali” anasema mkuu hiyo wa mkoa.
Mkuu huyo anaongeza kuwa anachokieleza Kwa Mkuu wa Wilaya hiyo ni kuhakikisha wanakaa na Mwekezaji huyo na warejee mazungumzo yao ya awali , kama kuna changamoto zirakazojitokeza pale katikati waangalie namna ya kuzifuta, na ” tukubaliane iwe ndani ya miezi miwili nataka muafaka wa hizi ekari 1,784 zinaendaje Kwa wananchi Kwa kuzingatia utaratibu, hekima na busara tulizonazo na si vinginevyo “
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Fakii Raphael Lulandala anasema amepokea agizo hilo, na ata hakikisha linakwenda kama ambavyo Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kufanyika.