Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed amewataka Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata mkoani Ruvuma kuona umuhimu wa kuwa na usikivu na udadisi katika kujifunza na kujadili masuala mbalimbali ambayo yatawawezesha katika utendaji wa majikumu yao ya kila siku.

Amesema uzoefu unaonyesha kuwepo changamoto zinazoathiri utoaji huduma kwa wananchi katika ngazi ya Kata na Tarafa zinazotokana na sababu mbalimbali.

Kanali Ahamed Abbasi Ahamed aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Maofisa Tarafa na watendaji wa Kata yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya manispaa ya Songea.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed akifungua mafunzo ya utawala Bora kwa maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata kutoka ofisi ya Rais Tamisemi yaliyofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Songea.

Alisema kuwa changamoto zinazotokea kwenye maeneo yao ya kazi ni pamoja na kutozingatia sharia ,Kanuni na Taratibu katika utendaji kazi wa kila siku ambapo alizitaja baadhi ya changamoto ni kuwepo kwa migogoro ya kiutendaji kati ya maofisa Tarafa, Watendaji wa kata,Wataalamu na Viongozi pamoja na wataalamu wengine katika ngazi hizo.

Alitaja changamoto zingine kuwa ni ufwatiliaji na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye ngazi za msingi,kutitatuliwa kwa wakati kero za wananchi pamoja na adau wengine katika ngazi za msingi, kutokuwa na uwelewa katika baadhi ya sera,sharia na miongozo wanayotakiwa kusimamia na kuitekeleza.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais Tamisemi Simon Maganga akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed afungue mafunzo ya siku mbili ya utawala Bora kwa maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata.

Alifafanuwa Zaidi kuwa changamoto nyingine ni kukosa ubunifu wa kiongozi katika usimamizi na uibuaji wa fursa za kichumi na kijamii zinazopatikana kwenye ngazi za msingipamoja na ushirikishaji wa wananchi na wadau wa maendeleo na kuwepo kwa changamoto za kimaadili ya kiutumishi kwa baadhi ya wataalam.

Mkuu wa Mkoa Kanali Ahamed amewakumbusha majukumu yao ya uofisa Tarafa na utendaji wa kata kua ni pamoja na kumwakilisha mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali kuu katika Tarafa ,kuhamasisha na kuhimiza maendeleo wananchi ili washiriki kwenye shughuli mbalimbali kwenye Tarafa walioko.

Pia kuwa kiungo kati ya Serika Kuu na wananchi katika ngazi ya Tarafa ,kushughulikia malalamiko ya wananchi na kufwatilia pamoja na kuwahimiza utekelezaji wa sera za serikali katika maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kuwa zinatekelzwa ipasavyo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya utawala Bora ambayo ni Watendaji wa Kata na Maofisa Tarafa wa Mkoa wa Ruvuma.

Alieleza zaidi kuwa ni pamoja na kushiriki na kutoa ushauri kuhusu upangaji wa mipango ya maendeleo katika maeneo yao ,mtendaji mkuu wa Kata ni kiungo cha uongozi kwa Idara zote ngazi ya Kata ,kuandaa mpango kazi wa maendeleo ya Kata na kuwakilisha kwa mkurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa ofisa Tarafa,kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera,Sheria,Kanuni na miongozo yz Serikali katika kata,mratibu na masimamizi wa upangaji wa mipango shirikishi ya maendeleo ya Kata, kupokea,kutatua malalamiko ya wananchi katika ngazi ya kata.

Mapema akimkaribisha mgeni rasmi mwakilishi wa mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais Tamisemi Simon Maganga alisema kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yanalenga katika kuwajengea uwezo Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata katika majukumu yao ya kila siku ukizingatia kwamba viongozi hao wapo karibu zaidi na wananchi katika maeneo ya Halimashauri na Vijiji hivyo ni vyema ofisi ya Rais Tamisemi ikawajengea uwezo wa majukumu yao ya kila siku kwa kuwa kunamabadiliko mbalimbali yamefanyika ya Sera ,mabadiliko ya watendaji wenyewe kuna baadhi wamepata nafasi hizi na wale ambao wanauzoefu basi kujuwa nini ambacho kwa sasa Serikali inatekeleza kutokana na majukumu yao ya kila siku.

Alisema kuwa mafunzo hayo ya Utawala Bora tayari yameshatolewa kwenye Mikoa 20 ya Tanzania na hivi sasa imebaki Mikoa sita ikiwemo Mkoa wa Ruvuma ambao unamaofisa tarafa 24 na Watendaji wa kata 179 ambao wanaendelea kupatiwa mafunzo hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed akifungua mafunzo ya utawala Bora kwa maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata mkoani Ruvuma.

Salma Mapunda Ofisa Tarafa waTarafa ya Ruvuma Wilaya ya Songea ameishukuru serikali kwa kuwaletea mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwambusha majukumu yao ya kila siku katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ikiewemo miradi ya ujenzi inayoendelea kwenye Tarafa zao mafunzo hayo yatawasaidia namna ya usimamizi wa miradi hiyo pamoja na ubora wa majengo ambayo wanayasimamia ndani ya tarafa zao.

Zuberi said Zuberi ofisa mtendaji wa kata ya Namwinyu wilayani Tunduru alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia namna ya kubuni vyanzo vipya vya mapato katika ngazi ya kata, kutatua kero za wananchi pamoja na uwajibikaji wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku pamoja na usimamizi wa shughuli mbalimbali za maendeleo na ufwatiliaji wa miradi inayoendelea kujengwa kwenye Kata inayotekelezwa na serikali.