Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed amejiandikisha leo kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma jambo ambalo limeonesha mfano mzuri wa umuhimu wa ushiriki wa viongozi katika mchakato wa uchaguzi .
Kanali Ahamed amehimiza wananchi kujiandikisha na kushiriki kikamilifu zoezi la uandikishwaji daftari la kupigia kura ambapo amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishwaji vilivyopo kwenye maeneo yao ili waweze kuwa na sifa za kuwachaguwa viongozi watakao waongoza na kuwaletea maendeleo.
’”Nitumie fursa hii kumshukuru na kumpongeza rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukuza Demokrasia nchini upigaji kura na uandikishaji huu ni ishara ya demokrasia hiyo ambayo yeye kama mwananchi namba moja anaienzi ndani ya taifa letu ‘’alisema mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa kanali Ahamed amewapongeza na kuwashukuru viongozi wa dini,wananchi pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya,Halmashauri na watendaji wote kwa maandalizi mazuri yaliyofanywa katika kutoa elimu lakini pia katika kufanya hamasa kwa maafisa wasafirishaji .
“lakini pia nivipongeze vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya hamasa na kuwahabarisha wananchi juu ya zoezi hilo la uandikishaji kwenye daftari la kupigia kura pamoja na viongozi wa dini na vyama kwa kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi “alisema Kanal Ahemed.
Wakati huohuo Mbunge viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jacklin Ngonyani Msongozi amewataka wananchi wote wajitokeze kujiandikisha kweye daftari la kupigia kura hili zoezi hilo lifanyike kwa uhakika na kila mmoja atakaye toka kwenye kituo cha kuandikisha aende akahamasishe nyumbani ili watu wajitokeze kwa wingi kwenda kujiandikisha kwa sababu kujiandikisha ni wajibu wake kama mwananchi na hiyo ndio itakuwa fursa ya kwenda kumchaguwa mwenyekiti wa mtaa umtakae na si vinginevyo.
Nae Mkurugenzi wa manispaa ya Songea Bashiru Muhoja alisema kuwa wanatarajia kuandikisha wananchi wasiopungua kwaajiri ya zoezi la kupigia kura wananchi laki moja na hamsini na sita ambao wataandikishwa kwenye vituo 190 katika manispaa hiyo.